Pata taarifa kuu

Gaza: Meli ya kwanza inayosheheni msaada wa chakula kutia nanga Cyprus

Wazo la kupitia Cyprus, iliyoko chini ya kilomita 400 kutoka pwani ya Israel, ili kupeleka misaada ya kibinadamu Gaza, lilikuwa likizunguka kwa miezi kadhaa, hata kama hakuna kitu kinachoonekana kusonga mbele. Lakini tangu siku ya Ijumaa Machi 8 na tangazo la rais wa Marekani kwamba Marekani itajenga bandari huko Gaza, mpango wa kweli umeanzishwa na Tume ya Ulaya na ofisi ya rais wa Cyprus.

Meli hiyo ya shirika la misaada la Open Arms inatia nanga inapojiandaa kusafirisha tani 200 za mchele na unga moja kwa moja hadi Gaza, kwenye bandari ya Larnaca, Cyprus, Ijumaa Machi 8, 2024.
Meli hiyo ya shirika la misaada la Open Arms inatia nanga inapojiandaa kusafirisha tani 200 za mchele na unga moja kwa moja hadi Gaza, kwenye bandari ya Larnaca, Cyprus, Ijumaa Machi 8, 2024. AP - Marcos Andronicou
Matangazo ya kibiashara

Meli ya kwanza kutoka shirika lisilo la kiserikali la Open Arms la Uhispania inatarajiwa kuondoka Larnaca, kusini mwa Cyprus, kupeleka chakula, maji na vifaa muhimu.

Iwapo mamlaka ya Israel itaendelea kuziba masikio matakwa ya jumuiya ya kimataifa ambayo inataka kufunguliwa kwa maeneo zaidi ya vivuko na Gaza, baadhi ya nchi zimechagua njia nyingine. Wakati Wapalestina wanasubiri chakula kwa hamu, wazo sasa ni kusafirisha msaada huu kutoka Cyprus, kupitia baharini, hasa kwa kutumia meli kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali la Uhispania la Open Arms.

Operesheni hii, iliyotangazwa siku ya Ijumaa Machi 8 na Rais wa Tume ya Ulaya, inategemea msaada wa Umoja wa Ulaya, Marekani, Cyprus na Falme za Kiarabu, kwa makubaliano ya mamlaka ya Israeli, bila yenyewe hakuna kitu kinachowezekana. Wazo ni kuleta msaada huu moja kwa moja kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuupakua kwa kutumia jahazi ambalo litavutwa njia nzima, kulingana na vyombo vya habari vya Uhispania.

tani 200 za msaada

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Open-Arms la Uhispania inapaswa kuondoka katika bandari ya Lanarca siku ya Jumapili Machi 10, kulingana na mamlaka ya Cyprus. Wizara ya Mambo ya Nje ya kisiwa hicho inahakikisha kwamba kilichobaki ni kutathmini hali ya hewa. Mchele, unga na protini zilipakiwa kwenye meli siku moja kabla, chini ya udhibiti wa waangalizi wa Israeli, kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini mwez Desemba mwaka uliyopita kati ya taifa la Kiyahudi na Cyprus.

Kwa jumla, mpango huu unapaswa kufanya uwezekano wa kusafirisha tani 200 za misaada, wakati hali ya Gaza ni janga kulingana na mashirika mengi yaliyopo huko. Mashirika haya wamekuwa yakibaini mara kwa mara kwamba misaada inayotolewa kwa ndege na ardhi haitoshi. Boti ya kwanza inapaswa kuwasili Jumapili hii huko Gaza, kulingana na Ursula von der Leyen, ambaye ameishukuru Open Arms na shirika lisilo la kiserikali la World Central Kitchen ambalo limekuwa likipambana kwa miezi miwili kuanzisha ukanda huu wa baharini.

Vizuizi vya majini viliwekwa Gaza tangu 2007

Iwapo World Central Kitchen itakuwa na jukumu la kusambaza misaada kutoka kwa msafara huu kwa Wapalestina, taratibu za upakuaji wa misaada kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo zinaendelea kubainishwa kutokana na hatari za kiusalama na ukosefu wa miundombinu. Siku ya Alhamisi, Machi 7, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza ujenzi wa "gati ya muda" kwenye pwani ya Gaza. Lakini kulingana na Pentagon, inaweza kuchukua hadi siku 60 na itahusisha maelfu ya askari.

Kwa upande wa Ulaya, michango kamili ya Tume, lakini pia ya Ujerumani, Italia na Uholanzi, bado haijafafanuliwa. Iwapo misafara hii ya baharini itaripotiwa, itakuwa ni mara ya kwanza kulegeza vizuizi vya majini vilivyowekewa Gaza na Israel tangu mwaka 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.