Pata taarifa kuu

Wito wa kusitishwa kwa mapigano kati ya Israeli na Hamas wazidi kutolewa

Nairobi – Wapatanishi wanaokutana mjini Cairo, Misri, kujadiliana kuhusu mpango wa usitishaji vita kati ya Israel na kundi la Hamas, wamezindua upya wito wao kwa pande hizo kuweka kando tofauti zao ili kupata muafaka, wakati huu majeshi ya Israel yakizidisha mashambulio zaidi.

Mapigano yamekuwa yakiendelea katika ukanda wa Gaza licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa
Mapigano yamekuwa yakiendelea katika ukanda wa Gaza licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa © AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano yalianza mwaka jana baada ya wapiganaji hao wa Palestina kutekeleza shambulio katika ardhi ya Israeli ambapo watu zaidi ya elfu moja waliuawa.

Wanadiplomasia wamekuwa wakishinikiza pande hizo kukubaliana mapema kabla ya kuanza kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Lakini je kuna uwezekano wowote wa makubaliano kufikiwa? Abdulkarim Atiki, ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania.

‘‘Israeli wao wana msimamo mkali na Hamas pia wana msimamo mkali ila wanaowapatanisha uwezo wao unaonekana kuwa mdogo.” alisema Abdulkarim Atiki.

00:57

Abdulkarim Atiki, ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania

Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris, amelitaka kundi la Hamas, kukubali mapendekezo ya usitishaji mapigano kwa wiki 6, ili kutoa nafasi ya misaada kufikishwa kwa maelfu ya raia walio katika hali mbaya kwenye eneo la Gaza.

‘‘Watu katika eneo la Gaza hawana chakula, hali ni ya kutisha na ubinadamu wetu wa pamoja unatulazimisha kuchukua hatua.’’ alieleza Makamu wa rais wa Marekani, Kamala Harris.

00:42

Makamu wa rais wa Marekani- Kamala Harris

Wito wake ameutoa wakati huu taifa lake likijiandaa kutumia ndege za kijeshi kudondosha misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula na madawa, kwa raia walionaswa kwenye mapigano.

Mapigano yamekuwa yakiendelea katika ukanda wa Gaza licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa, Israeli ikisema inawasaka wapiganaji wa Hamas.

Wizara ya afya inayoongozwa na Hamas inasema karibia watu 30,534 wameuwa katika mapigano kati yake na jeshi la Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.