Pata taarifa kuu

Wakaazi wengi wa Gaza wana majeraha ya risasi baada kushambuliwa na Israeli

Nairobi – Maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema wakaazi wengi wa Gaza wana majeraha ya risasi baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israeli walipokuwa wamekwenda kupokea msaada wa chakula.

Kundi ma Hamas limeishtumu Jeshi la Israeli kwa kuwapiga kwa makusudi, Wapalestina waliokuwa wamekwenda kupata msaada wa chakula
Kundi ma Hamas limeishtumu Jeshi la Israeli kwa kuwapiga kwa makusudi, Wapalestina waliokuwa wamekwenda kupata msaada wa chakula AP - Mahmoud Essa
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maafisa hao wa Umoja wa Mataifa, watu zaidi ya 200 wanapata matibabu kutoka na majeraha hayo, katika hospitali ya Al Shifa, baada ya tukio hilo ambalo lilisabisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 100 wiki hii.

Kundi ma Hamas limeishtumu Jeshi la Israeli kwa kuwapiga kwa makusudi, Wapalestina waliokuwa wamekwenda kupata msaada wa chakula.

Jamii ya kimataifa imelaani hatua ya jeshi la Israeli kuwashambulia raia wa Palestina
Jamii ya kimataifa imelaani hatua ya jeshi la Israeli kuwashambulia raia wa Palestina © Kosay Al Nemer / Reuters

Hata hivyo, Israeli imejitetea na kudai kuwa watu hao walikangayagana na kusababisha maafisa wake kupiga risasi za kutoa tahadhari, suala ambalo Jumuiya ya Kimataifa linataka uchunguzi huru kufanyika.

Wizara ya afya katika ukanda wa Gaza, limeonya kuwa maelfu ya wakaazi wa Kaskazini mwa Gaza, wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha kwa utapilia mlo na kuishiwa maji mwilini, iwapo hawatapata msaada wa haraka.

Viongozi wa dunia akiwemo rais Joe Biden wameikashifu Israeli kwa hatua hiyo
Viongozi wa dunia akiwemo rais Joe Biden wameikashifu Israeli kwa hatua hiyo REUTERS - ELIZABETH FRANTZ

Rais wa Marekani Joe Biden ambaye amesema ana matumaini kuwa, mkataba wa kusitisha vita kati ya Israeli na Hamas, utapatikana kufikia kuanza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jeshi la nchi yake, litatumia ndege kushusha misaada ya kkibinadamu kwa watu wa Palestina.

Katika hatua nyingine, ripoti zinasema Wapalestina 17 wameuawa na wengine wamejeruhiwa usiku kucha kufuatia mashambulio ya jeshi la Israeli yaliyolenga  maakazi ya watu kwenye maeneo ya Deir el-Balah na Jabalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.