Pata taarifa kuu

Mauaji ya watoto yanaendelea kwenye ukanda wa Gaza: Save the children

Nairobi – Shirika la kimataifa linalotetea haki za watoto la Save the Children linasema mauaji ya watoto yanaendelea kwenye ukanda wa Gaza kwa kiasi kikubwa, wakati huu jeshi la Israeli likiendelea kupambana na kundi la Hamas.

Watoto na wanawake ndio wameripotiwa kuathirika na mapigano yanayoendelea.
Watoto na wanawake ndio wameripotiwa kuathirika na mapigano yanayoendelea. REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

Alexandra Saieh, Mkuu wa Save the Children anayehusika na masuala ya sera katika shirika hilo, amesema kinachoendelea kwa sasa ni mauaji ya hatua kwa hatua ya watoto kwenye vita hivyo vinavyoendelea kushuhudiwa.

Kauli hii inakuja wakati huu wizara ya afya katika ukanda wa Gaza, ikisema watoto sita wameuawa kaskazini mwa eneo hilo kwa kukosa maji na utapia mlo, na wengine hali zao za afya ni mbaya.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa, watu zaidi ya laki tano, wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha kutokana na njaa kufuatia misaada ya kibinadamu kutowafikia wakaazi wa Gaza walioathiriwa na vita vinavyoendelea.

Katika hatua nyingine, idadi ya viveto vinavyotokana na vita vinavyoendelea imeongezeka na kufika zaidi ya elfu 30 kwa mujibu wa wiazara ya afya kwenye ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.