Pata taarifa kuu

Gaza: Lula alinganisha Israeli na Wanazi, Netanyahu akosoa 'kupuuzwa' kwa mauaji ya Holocaust

Rais wa Brazil ameishutumu siku ya Jumapili, Februari 18, Israel kwa "mauaji ya halaiki" na kulinganisha mashambulizi ya Israeli na kuangamizwa kwa Wayahudi na Wanazi. Matamshi haya makali yamezua hisia kali kutoka kwa Waziri Mkuu wa Israel, ambaye ameshutumu maneno "ya aibu na mazito", wakati akimwitisha balozi wa Brazil katika Wizara ya Mambo ya Nje huko Jerusalem.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akitoa tamko la kitaifa wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) huko Dubai, Falme za Kiarabu, Desemba 1, 2023.
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akitoa tamko la kitaifa wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) huko Dubai, Falme za Kiarabu, Desemba 1, 2023. REUTERS - THAIER AL-SUDANI
Matangazo ya kibiashara

 

Majibizano motomoto kati ya Luiz Inacio Lula da Silva na Benjamin Netanyahu baada ya Rais wa Brazil kushutumu Israel siku ya Jumapili, Februari 18, kwa kufanya "mauaji ya kimbari" ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akilinganisha mashambulizi ya Israel na kuangamizwa kwa Wayahudi na Wanazi. Waziri Mkuu wa Israel amejibu kwa kukashifu matamshi "ya aibu na mazito" na kumwitisha balozi wa Brazil nchini Israel siku ya Jumatatu, huku Waziri wake wa Ulinzi Yoav Gallant akiishutumu Brazil kwa "kuunga mkono" Hamas.

"Kinachotokea katika Ukanda wa Gaza sio vita, ni mauaji ya halaiki," Lula amewaambia waandishi wa habari kutoka Addis Ababa, Ethiopia, ambako mehudhuria mkutano wa Umoja wa Afrika. “Hivi si vita vya askari dhidi ya askari. Ni vita kati ya jeshi lililoandaliwa na wanawake na watoto. (...) Kinachotokea katika Ukanda wa Gaza na watu wa Palestina hakijatokea wakati mwingine wowote katika historia. Kwa kweli, hii tayari imetokea: wakati Hitler aliamua kuwaua Wayahudi, "amebainisha kiongozi wa Brazil, mkongwe wa mrengo wa kushoto.

Ulinganisho ambao "unavuka mstari mwekundu"

Kauli hizi ni miongoni mwa kauli mbaya zaidi kuwahi kutolewa kuhusu mzozo unaoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina na Lula, sauti maarufu kutoka Kusini ambayo nchi yake kwa sasa inashikilia urais wa zamu wa G20. Matamshi haya hayakuchelewa kujibiwa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye anasema ameguswa. "Maoni ya rais wa Brazil ni ya aibu na mazito," ameandika kweye ukurasa wake wa X. "Ni kupuuzia mauaji ya Holocaust na kujaribu kufutilia mbali raia wa kiyahudi na haki ya Israel kujilinda. Kulinganisha Israel na mauaji ya Nazi na Hitler anavuka mstari mwekundu,” ameongeza.

Waziri Mkuu wa Israel pia amesema kwamba "mara moja" amemwitisha balozi wa Brazil nchini Israeli "kuzungumza naye kuhusiana na matamshi ya rais wake". Waziri wa Mambo ya Nje, Israel Katz, amebainisha kwenye mtandao huo wa kijamii kwamba ataitishwa Jumatatu Februari 19. "Brazil imekuwa upande wa Hamas kwa miaka kadhaa. Rais Lula anaunga mkono kundi la kigaidi la mauaji ya halaiki (...) na kwa kufanya hivyo anatia aibu raia wake na kukiuka maadili ya ulimwengu huru," Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant amejibu kwenye mtandao wa X. Maoni haya pia yamezua hisia kali kutoka kwa mkurugenzi wa ukumbusho wa Holocaust, Yad Vashem, Dani Dayan. "Kulinganisha nchi inayopigana na kundi la kigaidi la mauaji na vitendo vya Wanazi wakati wa Maangamizi ya Wayahudi inastahili kulaaniwa," ameandika.

Kwa upande wake, Hamas "imekaribisha" katika taarifa kwa vyombo vya habari taarifa za Lula, ambazo kwa mujibu wake ni "maelezo kamili ya watu (wake) wanateseka" huko Gaza na kufichua "ukubwa wa uhalifu" uliofanywa na Israel "kwa msaada wa wazi wa utawala wa Biden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.