Pata taarifa kuu

Wanajeshi 24 wa Israeli wameuwa katika kipindi cha siku moja

Nairobi – Jeshi la Israel limethibitisha kuwapoteza maofisa wake wengi zaidi katika kipindi cha siku moja tangu kuanza kwa vita vyake vya ardhini huko Gaza huku kukiwa na shinikizo linalozidi kuitaka serikali kutafuta njia ya kumaliza mzozo huo.

Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakipambana na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza
Wanajeshi wa Israel wamekuwa wakipambana na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza via REUTERS - ISRAEL DEFENSE FORCES
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel, wanajeshi 24 waliuawa siku ya Jumatatu, wakati askari 21 wa akiba wakiuawa katika shambulio la roketi ya guruneti.

Mapigano hayo mazito yamekuja wakati huu ambapo afisa wa White House akitarajiwa kuwasili katika ukanda huo kwa mazungumzo zaidi yanayolenga kutafuta muafaka wa kuwaachia huru mateka zaidi.

Inahofiwa kuwa huenda mzozo kati ya Israel na Hamas ukasambaa hadi katika maeneo mengine ya Ukanda
Inahofiwa kuwa huenda mzozo kati ya Israel na Hamas ukasambaa hadi katika maeneo mengine ya Ukanda REUTERS - AMIR COHEN

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Marekani, Israel imependekeza kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa miezi miwili.

Shirika la misaada ya kibinadamu OCHA katika taarifa yake limeeleza kuwa mapigano na mashambulio yalishika kasi katika mji wa Khan Yunis kuisni mwa Gaza.

Aidha jeshi la Israel limeeleza kuwa maofisa wake wametekeleza mashambulio dhidi ya ngome za Hamas katika mji huo.

Mamia ya raia wa Gaza wametoroka katika makazi yao kwa kuhofia mashambulio ya Israel
Mamia ya raia wa Gaza wametoroka katika makazi yao kwa kuhofia mashambulio ya Israel REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Karibia raia milioni 1.7 wameripotiwa kupoteza makazi yao katika ukanda wa Gaza, Mashirika ya misaada yakionya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa baa la njaa na magonjwa.

Makabiliano kati ya Israel na Hamas yalianza tarehe 7 ya mwezi Oktoba mwaka wa 2023 baada ya wapiganaji hao kutekeleza shambulio dhidi ya Israel ambayo kwa mujibu wa mamlaka lilisababisha vifo vya karibia watu 1,140.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.