Pata taarifa kuu

Marekani na Uingereza zatekeleza mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi

Nairobi – Marekani na Uingereza zimefanya mashambumlio mapya hapo jana kuwalenga waasi wa Houthi wa nchini Yemen, wanaoungwa mkono na Iran, katika hatua ya kujibu mashambulio ya waasi hao katika bahari nyekundu.


Vikosi vya marekani na Uingereza vilitekeleza mashmabulio ya kwanza dhidi ya kundi hilo mapema mwezi huu
Vikosi vya marekani na Uingereza vilitekeleza mashmabulio ya kwanza dhidi ya kundi hilo mapema mwezi huu AP - AS1 Jake Green RAF
Matangazo ya kibiashara

 

Vikosi vya marekani na Uingereza vilitekeleza mashmabulio ya kwanza dhidi ya kundi hilo mapema mwezi huu, marekani nayo ikizidisha mashambulio zaidi ya anga dhidi ya makombora ambayo Washington ilisema inatishia meli za raia na kijeshi.

Mashambulio ya hivi punde ya Marerkani na Uingereza, yalilenga maeneo  ya Houthi nchini Yemen, kutokana na mashambulio ya Houthi dhidi ya meli za kimataifa na kibiashara, na yananuia kudhoofisha uwezo wa waasi hao unaotishia biashara ya kimataifa.

Hata hivyo waasi wa Houthi wameapa kuendelea na mashambulio yao, katika moja ya mzozo, unaohusishwa na vita vya Israel na Hamas ambavyo vimeongeza hali ya wasiwasi katika eneo la mashariki ya kati.

Mapema jumatau, waasi wa Houthi walidai kuishambulia meli ya mizigo ya Marekani pwani ya Yemen, msemaji wao yahya Saree akisema waliongoza oparesheni ya kijeshi kulenga meli ya mizigo ya kijeshi ya Marekani karibu na bahari nyekundu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.