Pata taarifa kuu

Palestine: Raia wengi wameendelea kuuawa katika vita vya Israel na Hamas

Nairobi – Vita kati ya Jeshi la Israeli na kundi la Hamas kwenye ukanda wa Gaza, vimeingia kwa siku ya 100, wakati huu raia wengi wakiendelea kuuawa, huku mateka kutoka Israel wakiendelea kushikiliwa.

Près des décombres d'une maison détruite par une frappe israélienne à Rafah, dans le sud de la bande de Gaza, le 9 janvier 2024.
Près des décombres d'une maison détruite par une frappe israélienne à Rafah, dans le sud de la bande de Gaza, le 9 janvier 2024. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa, unasema, hali ya ukanda wa Gaza, inaendelea kuwa mbaya, asilimia 85 ya wakaazi wa eneo hilo hawana tena makao na wanakosa mahitaji muhimu ya kibinadamu kama chakula, dawa na nishati.

Vita vilivyoanza Oktoba tarehe 7 mwaka uliopita, baada ya kundi la Hamas kuvamia Kusini mwa Israel na kusababisha viveo vya watu wapatao 1,140, ​​​​vimesababisha viveo vya watu karibu Elfu 24 sasa, kwenye ukanda wa Gaza, wengi wakiwa raia wa kawaida.

Jeshi la Israeli linasema vita hivi vitaendelea kwa miezi kadhaa ijayo, wakati huu likisisitiza kufanikiwa kuondoa kabisa ngome ya kundi la Hamas, Kaskazini mwa Gaza, katika vita ambavyo vinahofiwa kuwa, huenda vikawa vya kikanda.

Jeshi la Israeli limeripotiwa katika kipindi hiki cha siku 100 likipambana na wapiganaji wa Hezbollah katika mpaka wa nchi ya Lebanon, huku naibu kamanda wa kundi hilo akiuawa siku kadhaa zilizopita.

Kundi la Hamas, limeonesha mkanda wa video ukiwaonesha mateka watatu wakiwa kizuizini, wakionekana wakizungumza kwa Kiebrania, wakiitaka Israel kuwarudisha nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.