Pata taarifa kuu

Israel imetakiwa kuruhusu misaada kuingia Gaza kupitia bandari ya Ashdod

Nairobi – Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yametoa wito kwa kwa Israel kuruhusu misaada ya dharura ya kibinadamu kuingia Kaskazini mwa Gaza kupitia katika bandari ya Ashdod.

Wito wa UN unakuja wakati huu ambapo vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hamas vikiingia katika siku ya 100
Wito wa UN unakuja wakati huu ambapo vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hamas vikiingia katika siku ya 100 Jack GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya WHO, WFP na UNICEF kupitia taarifa ya pamoja yamesema  raia katika Ukanda wa Gaza wanahitaji kwa dharura msaada wa chakula na bidhaa nyengine kama njia moja ya kukabiliana na athari inayoongezeka ya kutokea kwa baa la njaa.

Wito wa UN unakuja wakati huu ambapo vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hamas vikiingia katika siku ya 100, pande hasimu zikiendelea kupokea shinikizo ya kusitisha mapigano yanayoendelea.

UN inasema raia katika Ukanda wa Gaza wanahitaji misaada kwa dharura
UN inasema raia katika Ukanda wa Gaza wanahitaji misaada kwa dharura REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA

Kutokana na makabiliano hayo, zaidi ya raia 2.4 katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na changamoto ya kupata huduma muhimu kama vile maji, chakula, mafuta na huduma za matibabu.

Kwa mujibu wa mkurungenzi mkuu wa WFP katika ukanda wa Mashariki ya kati, hatua ya kufunguliwa kwa bandari ya Ashdod itasaidia kupunguza muda wa kuwasilisha msaada kwa raia wa Gaza kutokea katika eneo la Kaskazini.

Mapigano kati ya Hamas na Israel yameingia siku ya 100
Mapigano kati ya Hamas na Israel yameingia siku ya 100 REUTERS - TYRONE SIU

Mwezi Desemba, Israel iliidhinisha mpango wa muda wa kupeleka chakula katika Ukanda wa Gaza kupitia kwa mpaka wa Kerem Shalom kusini wa Gaza baada ya majuma kadhaa ya shinikizo la jamii ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.