Pata taarifa kuu

Lebanon: Kamanda wa juu wa kundi la Hezbollah ameauwa

Nairobi – Kamanda wa juu wa kundi la Kiislamu la Hezbollah nchini Lebanon, ameauwa baada ya kushambuliwa na ndege ya kivita isiyokuwa na rubani ya Israeli.

Kuuawa kwa viongozi hao wa Hezbollah, kunazua wasiwasi kuwa vita kati ya Jeshi la Israeli na kundi la Hamas
Kuuawa kwa viongozi hao wa Hezbollah, kunazua wasiwasi kuwa vita kati ya Jeshi la Israeli na kundi la Hamas AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, shambulio hilo lilimlenga Kamanda huyo wa Hezbolla akiwa kwenye msafara wa magari katika eneo la Khirbet Selm, Kusini mwa Lebanon.

Kuuawa kwa Kamanda huyo kunakuja baada ya naibu kiongozi wa Hezbollah Saleh al-Aruri, kuuawa wiki iliyopita, baada ya kushambuliwa na jeshi la Israeli, jijini Beirut.

Kuuawa kwa viongozi hao wa Hezbollah, kunazua wasiwasi kuwa vita kati ya Jeshi la Israeli na kundi la Hamas, huenda vikasambaa na kuwa vya kikanda.

Hezbollah imeapa kulipiza kisasa dhidi ya mauaji ya kamanda wa Hamas
Hezbollah imeapa kulipiza kisasa dhidi ya mauaji ya kamanda wa Hamas ASSOCIATED PRESS - Hussein Malla

Tangu kuanza kwa vita hivyo, Oktoba 7, jeshi la Israeli limekuwa likishambuliana na Hezbollah katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

Kundi la Hezbollah limeapa kulipiza kisasi dhidi ya kuuawa kwa viongozi wake, na Jumamosi iliyopita, Mkuu wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell alikutana na afisa wa juu wa kisiasa wa Hezbollah kwa ajili ya mazungumzo yaliyolenga kuzuia Lebanon kuingozwa kwenye vita kati ya Israel na Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.