Pata taarifa kuu

Jeshi la Israeli laendelea kushambulia Gaza, UN yahofia usalama wa raia

Wanajeshi wa Israel wameendelea kurusha mabomu katika ukanda wa Gaza, wakati huu mashambulio yakionekana kulenga zaidi maeneo ya Kusini, ambako kuna maelfu ya wakimbizi.

Shambulio la jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza
Shambulio la jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza REUTERS - VIOLETA SANTOS MOURA
Matangazo ya kibiashara

Wiki hii mji wa Khan Yunis, ulio Kusini mwa Gaza, umeshuhudia mashambulio mazito ikiwemo siku ya Alhamisi, jeshi la Israeli likisema linawasaka wapiganaji wa kundi la Hamas.

Wizara ya afya katika ukanda wa Gaza  inasema, watu wengine 50 wameuawa leo na wengine wakaachwa na majeraha, baada ya jeshi la Israeli kushambulia maeneo ya Beit Lahiya, Khan Younis na Maghazi.

Aidha, jeshi la Israeli linaripotiwa kuongeza vikosi vyake katika mji wa Khan Yunis, nyumbani kwao kiongozi wa Hamas, Yahya Sinwar.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kukabiliana na hali mbaya inayoendelea kuwakumba watu wa Gaza.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, amesema  jeshi la Israeli linapoendelea na operesheni yake, lisiwalenge raia wasiokuwa na hatia.

Nayo Tume ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia masuala ya haki za binadamu, katika ripoti yake, imesema jeshi la Israeli limeendelea kutekeleza mauaji ya Wapalestina wasiokuwa na hatia, kinyume cha sheria.

Tangu tarehe 7 mwezi Oktoba, watu zaidi ya Elfu 21 wameauwa katika mashambulio ya jeshi la Israeli kwenye ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.