Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel laendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza, nchi za kiarabu zapaza sauti

Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumapili, Novemba 5 usiku kwamba linaendelea na "mashambulizi makubwa" ambayo "yataendelea katika siku zijazo" katika Ukanda wa Gaza, na kuongeza kuwa imeligawanya eneo la Palestina katika sehemu mbili.

Moshi na miali ya moto kuongezeka kutoka Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi mapya ya Israeli, Novemba 5, 2023.
Moshi na miali ya moto kuongezeka kutoka Ukanda wa Gaza baada ya mashambulizi mapya ya Israeli, Novemba 5, 2023. REUTERS - RONEN ZVULUN
Matangazo ya kibiashara

"Mashambulizi makubwa sasa yanaendelea ... na yataendelea usiku wa leo na katika siku zijazo," msemaji wa jeshi Daniel Hagari amesema, akisisitiza kwamba vikosi vya Israeli vinavyofanya kazi katika eneo hilo vimegawanyika katika sehemu mbili: "Gaza Kusini na Gaza Kaskazini".

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefutilia mbali usitishwaji wowote wa mapigano hadi mateka wa Hamas watakapoachiliwa. Jeshi la Israel linaonya kwamba "mashambulio makubwa" yataendelea katika siku zijazo huko Gaza, eneo ambalo sasa limegawanywa mara mbili kati ya "Gaza Kusini na Gaza Kaskazini".

Hayo yanajiri wakati watu wanne wa familia ya mwandishi wa habari wa Lebanon, watoto watatu na mwanamke mmoja, waliuawa na shambulio la Israeli kwenye gari lao kusini mwa Lebanon. Katika kulipiza kisasi, Hezbollah ilirusha makombora huko Kiryat Shmona, kaskazini mwa Israeli, na inatarajia kuwasilisha malaalmiko yake kwa Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken alikutana na Mahmoud Abbas. Rais wa Mamlaka ya Palestina alishutumu "mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na Israel " katika Ukanda wa Gaza. Alisema "mapigano yanapaswa kusitishwa mara moja" na misaada ya kibinadamu inapaswa kuingia Ukanda wa Gaza.

Zaidi ya watu 45 waliuawa na karibu mia wengine kujeruhiwa katika hujuma ya Israel dhidi ya kambi ya wakimbizi ya Maghazi Jumamosi jioni, katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Tangu Oktoba 7, zaidi ya Waisraeli 1,400 waliuawa, wakiwemo wanajeshi 341, na jeshi la Israel linaripoti watu 240 wanaoshikiliwa mateka na Hamas. Wizara ya Afya ya Hamas imetangaza idadi ya vifo vya Wapalestina 9,770, wakiwemo watoto 4,800.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.