Pata taarifa kuu

Waandishi wa habari kumi na sita wa Kipalestina wameuawa tangu kuanza kwa vita Gaza

Waandishi wa habari 16 wa Kipalestina wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na Hamas, vilivyochochewa baada ya shambulio la kundi la wanamgambo wa Kiislamu katika ardhi ya Israel Oktoba 7, muungano wa waandishi wa habari wa Palestina umesema Alhamisi, Oktoba 19.

Wakati wa maandamano ya kuunga mkono Palestina, Oktoba 18, 2023.
Wakati wa maandamano ya kuunga mkono Palestina, Oktoba 18, 2023. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, chama hicho chenye makao yake katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, kilikadiria kuwa makumi ya wengine wamejeruhiwa. Takriban watu 3,785 wameuawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza, kulingana na mamlaka ya Palestina.

Wakati huo huo Waziri wa ulinzi wa Israel amekutana na wanajeshi wa Israel katika mpaka wa Gaza mapema siku ya Alhamisi.

Yoav Gallant alivitaka vikosi "kujipanga, kuwa tayari", kulingana na shirika la habari la AP."

Yeyote anayeiona Gaza kwa mbali sasa, ataiona kutoka ndani," alisema. "Israel imekusanya makumi ya maelfu ya wanajeshi kwenye mpaka."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.