Pata taarifa kuu

Marekani kushirikiana na Israel kuhakikisha raia zaidi hawauawi kwenye êneo la Gaza

NAIROBI – Rais wa Marekani, Joe Biden, amesema nchi yake itashirikiana kwa karibu na Israel, kuhakikisha raia zaidi hawauawi kwenye êneo la Gaza, wakati huu Tel Aviv, ikizidisha mashambulio dhidi ya Hamas. Biden ametoa kauli hii katika mkutano wake na waziri mkuu Benjamini Netanyahu

Joe Biden, amesema nchi yake itashirikiana kwa karibu na Israel, kuhakikisha raia zaidi hawauawi kwenye êneo la Gaza, wakati huu Tel Aviv, ikizidisha mashambulio dhidi ya Hamas
Joe Biden, amesema nchi yake itashirikiana kwa karibu na Israel, kuhakikisha raia zaidi hawauawi kwenye êneo la Gaza, wakati huu Tel Aviv, ikizidisha mashambulio dhidi ya Hamas via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Licha ya kutoilaumu moja kwa moja nchi ya Israel kwa shambulio lililolenga hospital mjini Gaza, Biden, ameitaka nchi hiyo kutekeleza operesheni zake kwa umakini kuepusha madhara zaidi kwa raia.

“Ninataka ufahamu hauko peke yako, hauko peke yako kabisa, kama nilivyosisitiza awali tuatendelea kusimama na Israeli.” alisema rais Biden.

00:17

Rais Biden kuhusu Israeli

Kwa upande wake, waziri mkuu Benjamin Netanyahu, amedai kundi la Hamas ndilo limehusika na shambulio kulenga hospitali, akisisitiza kuwa majeshi yake yatawasaka wapiganaji wa kundi hilo kokote walipo.

“Israeli itafanya kile inachoweza kuwalinda raia, tumewataka waende katika maeneo salama.” alisema Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

00:23

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Aidha katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, mbali na kukashifu shambulio dhidi ya Hospitali, amesisitiza wito wa kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada kuwafikia raia waliokwama Gaza.

“Nasikitishwa na mamia ya watu waliouawa katika shambulio dhidi ya hosipitali, natoa wito wa usitishwaji wa mapigano.” alisema katibu mkuu wa UN.

 

Ziara ya Biden nchini Israel, imekuja saa chache tangu nchi za kiarabu zitangaze kusitisha mkutano wao na Marekani, ambayo inajaribu kuzishawishi nchi hizo kulilaani kundi la Hamas.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.