Pata taarifa kuu

Iran yaongeza shinikizo kwa Israel na Marekani, na hivyo kuongeza tishio la kuzuka vita vipya

Pamoja na kuanza tena kwa mzozo wa Israel na Palestina tangu Jumamosi ya wiki iliyopita, Iran iko katikati ya tahadhari zote kwa uungaji mkono wake usio na kikomo kwa Hamas.

Waziriwa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amekariri kwamba washirika wa kikanda wa Iran (Syria, Hezbollah, Hamas, miongoni mwa wengine), wanaojulikana kwa njia isiyo rasmi kama "Mhimili wa Upinzani," wanaweza kujibu ikiwa mashambulizi ya Israel hayatasitishwa huko Gaza.
Waziriwa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amekariri kwamba washirika wa kikanda wa Iran (Syria, Hezbollah, Hamas, miongoni mwa wengine), wanaojulikana kwa njia isiyo rasmi kama "Mhimili wa Upinzani," wanaweza kujibu ikiwa mashambulizi ya Israel hayatasitishwa huko Gaza. AFP - JOSEPH EID
Matangazo ya kibiashara

Ingawa Tehran kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono kundi hili la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina, viongozi wa Iran hata hivyo wanadai kutohusika katika shambulio lililoanzishwa Jumamosi dhidi ya Israel, adui mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ijumaa hii, Oktoba 13, mkuu wa diplomasia ya Iran, Hossein Amir-Abdollahian, ametangaza kwamba Marekani "inapaswa kuidhibiti Israel" ikiwa wanataka kuepuka vita vya kikanda.

"Marekani inataka kuiruhusu Israel kuharibu Gaza na hilo ni kosa kubwa. Iwapo Wamarekani wanataka kuzuia vita visiedelei katika eneo hilo, lazima wadhibiti Israel,” amewaambia wanahabari wakati wa ziara yake huko Beirut, nchini Lebanon. "Ikiwa uhalifu wa Israeli hautakomeshwa, hatujui nini kitatokea," ameonya.

Waziri huyo, hata hivyo, amesisitiza kwamba "usalama na amani nchini Lebanon ni muhimu kwetu", huku kukiwa na hofu kubwa ya kuona Hezbollah ya Lebanon, mshirika wa Iran, ikifungua vita vipya dhidi ya Israel.

Marekani inahofia kufunguliwa kwa vita vyya pili kaskazini mwa Israeli kwenye mpaka na Lebanon, ikiwa Hezbollah itaamua kuingilia kati kwa nguvu. Kwa sasa, tangu kuanza kwa vita mnamo Oktoba 7, ushiriki wa Hezbollah kutoka kusini mwa Lebanon umebakia tu kwenye mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za Israeli huko kakazini, yenye lengo la kusaidia Hamas.

Wakati wa ziara yake huko Beirut, mkuu wa diplomasia ya Iran pia amekutana na kiongozi wa Hezbollah. "Wameshauriana kuhusu majukumu ambayo yanawahusu wote, na misimamo ambayo lazima ichukuliwe kutokana na matukio ya kihistoria na matukio ya hivi punde," taarifa ya Hezbollah kwa vyombo vya habari imesema baadaye.

Hossein Amir-Abdollahian amekariri kwamba washirika wa kikanda wa Iran (Syria, Hezbollah, Hamas, miongoni mwa wengine), wanaojulikana kwa njia isiyo rasmi kama "Mhimili wa Upinzani," wanaweza kujibu ikiwa mashambulizi ya Israel hayatasitishwa huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.