Pata taarifa kuu

Israeli: Mahakama imesikiliza kesi kuhusu namna ya kumuondoa waziri mkuu afisini

Mahakama ya rufa nchini Israeli, imesikiliza rufa kuhusu namna ambavyo waziri mkuu anaweza kuondolewa afisini, hatua inayokuja wakati huu maandamano yakishuhudiwa dhidi ya utawala wa waziri mkuu wa sasa Benjamin Netenyahu kwa kutekeleza mageuzi katika idara ya Mahakama.

Chini ya sheria hiyo, waziri mkuu anaweza tu kuondoka madarakani iwapo ataridhia au ikiwa theluthi tatu ya wabunge wengi wataunga mkono kuondolewa kwake
Chini ya sheria hiyo, waziri mkuu anaweza tu kuondoka madarakani iwapo ataridhia au ikiwa theluthi tatu ya wabunge wengi wataunga mkono kuondolewa kwake © Abir Sultan / AP
Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo inasikilizwa wakati huu Israeli ikikabiliwa na joto la kisiasa kuhusu mageuzi ya idara ya mahakama, mpango ambao umesababisha maandamano makubwa kwenye taifa hilo.

Majaji kumi na mmoja kati ya kumi na watano wa mahakama ya rufa wamesikiliza rufa tatu dhidi ya sheria hiyo iliyopitishwa mwezi Machi ikiwa ni sehemu ya mabadiliko katika mojawapo ya sheria kuu katika taifa hilo.

Chini ya sheria hiyo, waziri mkuu anaweza tu kuondoka madarakani iwapo ataridhia au ikiwa theluthi tatu ya wabunge wengi wataunga mkono kuondolewa kwake.

Kabala ya kuuanza kusikilizwa kwa rufa hiyo, mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya makaazi ya waziri mkuu Netanyahu jijini Jerusalem, hatua iliyopelekea kukamtwa kwa watu wanne kwa mujibu wa polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.