Pata taarifa kuu

Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA nchini Saudi Arabia: timu ya Israeli yawasli Riyadh

Zaidi ya miaka hamsini iliyopita, ni diplomasia kubwa iliyowezesha maelewano kati ya Marekani na Jamhuri ya Watu wa China. Wakati huu, ni Saudi Arabia na Israeli ambazo zinafanya jitihada hizi. Nchi hizo mbili hazina uhusiano wa kidiplomasia. Lakini, Riyadh inapokea timu ya wanamichezo ya Israeli.

Hii ni kwa mara ya kwanza: timu ya wachezaji wa Israel imetua Riyadh. Watashiriki wiki ijayo katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA.
Hii ni kwa mara ya kwanza: timu ya wachezaji wa Israel imetua Riyadh. Watashiriki wiki ijayo katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA. © AFP - DAVID MCNEW
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul

Hii ni kwa mara ya kwanza: timu ya wachezaji wa Israel imetua Riyadh. Watashiriki wiki ijayo katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA. Haya ni mashindano ya kimataifa ya mchezo wa video wa kandanda yaliyoandaliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Saudi Arabia iliahidi kuzikaribisha timu zote, bila kujali asili yao, lakini haikuitaja Israeli hasa. Inasemekana Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, ndilo lililoandaa safari hii bila ya kuwepo mawasiliano ya moja kwa moja kati ya serikali ya Israel na Saudia.

Mvutano watanda kwenye mahusiano yaliyokwama

Kikosi cha Israel kina wachezaji watatu, kocha na meneja. Waliwasili nchini kupitia Umoja wa Falme za Kiarabu wakiwa na pasi za kusafiria za Israel. Tangu kuwasili kwao, wamefanya mahojiano mengi, hasa na vyombo vya habari nchini Israeli ambapo walionekana wakivaa mashati ya timu ya taifa.

Tukio hili linakuja wakati kuna mazungumzo ya juhudi za kufufua uhusiano kati ya Israeli na Saudi Arabia chini ya mwamvuli wa Marekani. Mtazamo ambao umekuwa mbali kwa kiasi fulani kutokana na mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.