Pata taarifa kuu

Uturuki na Misri kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia

Uturuki na Misri zimeteua mabalozi ili kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili katika ngazi ya juu ya kidiplomasia.

Uturuki na Misiri kuwateua mabalozi kila upande
Uturuki na Misiri kuwateua mabalozi kila upande AP - Burhan Ozbilici
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki siku ya Jumanne, Cairo na Ankara zilisema Uturuki ilimteua Salih Mutlu Sen kuwa balozi wake mjini Cairo na Misri kwa upande wake ilimteua Amr Elhamamy kuwa balozi wake mjini Ankara.

"Hatua ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ilitekelezwa kwa mujibu wa uamuzi uliochukuliwa na marais wa nchi hizo mbili," ilisema taarifa hiyo.

"Hatua hii inalenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na inaonyesha nia ya pande zote ya kuboresha uhusiano wa nchi mbili kwa maslahi ya watu wa Uturuki na Misri."

Uturuki na Misiri zimekuwa zikitofautiana katika masuala tofauti ambapo viongozi wa nchi hizo wameonekana wakishambuliana kwa matusi hadharani, kabla ya kuingia katika mchakato wa kurejesha uhusiano mwaka wa 2020.

Mataifa hayo mawili yamekuwa na mazungumzo katika ngazi ya mawaziri kwa mara kadhaa mwaka 2023 wakijadiliana kwa uwazi juu ya kuanzisha tena uhusiano kamili wa kidiplomasia.

Maafisa wakuu wa wizara ya mambo ya nje kutoka pande hizo mbili wamefanya mazungumzo tangu mwaka 2021 huku Ankara ikizindua mpango wa sera ya kigeni wa kurekebisha uhusiano na mataifa mengine yenye nguvu katika ukanda, kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu, Israel na Saudi Arabia pamoja na Misri.

Juhudi za maelewano kati ya Uturuki na Misri zilichukua mkondo muhimu baada ya Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na mwenzake wa Uturuki Tayyip Erdogan kusalmiana kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar mwishoni mwa 2022

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.