Pata taarifa kuu

Saudi Arabia kupunguza uzalishaji wa mafuta, Urusi kupunguza uuzaji nje ya nchi

Nairobi – Saudi Arabia imesema itapunguza uzalishaji wa mafuta kwa hiari kwa mapipa milioni moja kwa siku, hatua inayokuja baada ya Urusi, kusema itapunguza mauzo yake ya nje kwa mapipa 500,000. 

Saudi Arabia kupunguza uzalishaji wa mafuta, Urusi kupunguza uuzaji nje ya nchi
Saudi Arabia kupunguza uzalishaji wa mafuta, Urusi kupunguza uuzaji nje ya nchi AP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imeonekana kama jaribio jingine kutoka kwa wazalishaji wakubwa wa mafuta kuimarisha masoko yaliyotikiswa na masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kudorora kwa uchumi wa China. 

Saudi Arabia , muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta ghafi duniani, ilitangazwa kwa mara ya kwanza baada ya mkutano wa mwezi Juni mwaka huu ambapo nchi zinazozalisha mafuta kwa uwingi ziliridhia kupunguza uzalishaji wa siku.

Katika taarifa yake, Saudi Arabia imesema hatua hiyo itaendelea hadi mwezi Agosti kukiwa na uwezekano wa kuongeza muda.

Baada ya tangazo hilo, taifa hilo la Mashariki ya kati linasalia na uzalishaji wa mafuta wa mapipa milioni tisa kwa siku.

Kando na Saudi Arabia, Urusi nayo imetangaza kupunguza uuzaji wa mafuta yake nje ya nchi kwa mapipa laki tano kama njia moja ya kuhakikisha kuwa masoko ya mafuta ya ndani yanakuwa sawa. 

Tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Moscow imekuwa ikishuhudia mabadiliko ya uuzaji wa nishati yake katika bara Ulaya, India na China. 

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya uchumi, hatua hii huenda ikasababisha kupanda kwa bei ya mafuta au bei ya sasa kusalia kama ilivyo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.