Pata taarifa kuu
IMANI-DINI

Makka: Maelfu ya waumini wakusanyika kwa ajili ya kuanza kwa ibada ya Hija

Zaidi ya waumini milioni 2 wa Kiislamu, kutoka nchi 160, wanatarajiwa katika mji  mtakatifu wa Makka kutekeleza ibada hii ya Hija, ambayo ni moja ya nguzo tano za Uislamu.

Waislamu wakisali katika Msikiti Mkuu wakati wa Hija ya kila mwaka katika mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia.
Waislamu wakisali katika Msikiti Mkuu wakati wa Hija ya kila mwaka katika mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia. REUTERS - Waleed Ali
Matangazo ya kibiashara

Tukio kubwa la kiroho kwa mamilioni ya Waislamu, Hija imeanza Jumapili hii, Juni 25 huko Makka, nchini Saudi Arabia. Mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu, kikomo cha idadi ya mahujaji kilichowekwa wakati wa mzozo wa kiafya kimeondolewa. Kwa hivyo mamia ya maelfu ya watu tayari wako Makka, kulingana na shirika la habari la AFP. Kwa jumla, zaidi ya waumini milioni 2 kutoka nchi 160 wanatarajiwa katika mji huo mtakatifu kutekeleza ibada ya Hija, ambayo ni moja ya nguzo tano za Uislamu.

Ni hatua muhimu kwa Mwislamu yeyote muaminifu ambaye ana uwezo wa kuitekeleza. Hija inajumuisha mfululizo wa ibada zinazopaswa kufanywa katika mji mtakatifu na vitongoji vyake. Kuanzia Jumamosi, mahujaji walianza tawaf - mfululizo wa ibada - kuzunguka Kaaba, jengo takatifu la ujazo lililofunikwa kwa hariri nyeusi, lililoko karibu na katikati ya Msikiti Mkuu huko Makka. Ni kwa Kaaba, iliyojengwa katika karne ya 7, ambapo Waislamu ulimwenguni kote wanageukia kutekeleza sala zao za kila siku.

Jumapili hii jioni, mahujaji wanatarajia kwende Mina, mji unaopatikana kilomita 5 kutoka Msikiti Mkuu, kabla ya kufika Mlima Arafat - mahali pa mahubiri ya mwisho ya Mtume Muhammad (SW) - kutekeleza ibada kuu.

Changamoto kubwa kwa Saudi Arabia

Kwa gharama ya dola 5,000 kwa kila mtu, safari hiyo inaingiza mabilioni ya dola kwa mwaka kwa Saudi Arabia kila mwaka kabla ya janga Uviko. Changamoto kubwa kwa nchi hii ya Mashariki ya Kati ambayo ushawishi wake mara kwa mara umechafuliwa na ripoti yake wa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, na kupanda kwa joto - ndani ya nchi inakaribia nyuzi 45 - kumebadilika na kuwa changamoto katika miaka ya hivi karibuni. Kwa hiyo mfumo wa dharura ulioimarishwa unapangwa ndani ya Msikiti Mkuu ili kuhakikisha afya njema na usalama wa mahujaji.

Blinken anasema uasi wa muda mfupi kutoka kwa mamluki wa Wagner unaonyesha "mpasuko halisi" katika mamlaka ya Putin, kulingana na shirika la habari la AFP.

Uasi wa kundi la kibinafsi la mamluki na kiongozi wake Yevgeny Prigozhin mwishoni mwa juma ulikuwa "pingamizi ya moja kwa moja kwa mamlaka ya Putin", Blinken amesema.

"Kwa hivyo hii inazua maswali mazito, inaonyesha mpasuko halisi," Blinken aliambia kipindi cha mazungumzo cha CBS News 'Face the Nation'.

Ni mapema mno kusema nini mustakabali wa kundi la mamluki la Wagner walioasi jana, Blinken anasema.

Kama tumekuwa tukiripoti, Kremlin imesema haitowafungulia mashtaka wanajeshi wa Wagner ambao waliasi jana, licha ya kuwashutumu mapema kwa uasi wa kutumia silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.