Pata taarifa kuu

Saudia: Mwanamfalme Mohamed bin Salman aanza ziara ndefu ya kiserikali nchini Ufaransa

Mrithi wa Kifalme mwenye ushawishi mkubwa nchini Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, anaanza ziara ndefu nchini Ufaransa leo Jumatano, ambapo atakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ambaye anajaribu kuzishawishi nchi zinazoinukia kulaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine na kuunga mkono mkataba mpya wa kifedha".

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimkaribisha Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman alipowasili katika Ikulu ya Elysée mjini Paris Julai 28, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimkaribisha Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman alipowasili katika Ikulu ya Elysée mjini Paris Julai 28, 2022. AFP - BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa atampokea kiongozi mkuu wa nchi hii tajiri kwa mafuta siku ya Ijumaa wakati wa chakula cha mchana huko Élysée, kulingana na wasaidizi wake. Mwanamfalme, aliyepewa jina la utani "MBS" na mmiliki wa makazi ya kifahari yaitwayo Château Louis XIV, karibu na Versailles, katika mkoa wa Paris, atashiriki katika Mkutano wa Mkataba mpya wa kifedha wa kimataifa, ulioandaliwa na Emmanuel Macron mnamo Juni 22 na 23 huko Paris, kwa upande wake, mamlaka nchini  Saudi Arabia imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari ikitangaza kuwa "ziara hii ni ya kiserikali".

Mwezi Julai mwaka huu, wakati wa ziara ya hapo awali ya Mohammed ben Salman huko Paris, rais na mwanamfalme walihakikisha kwamba wanataka kushirikiana ili "kupunguza athari" za mzozo huo. Watetezi wa haki za binadamu na mrego wa kushoto nchini Ufaransa walimshutumu Emmanuel Macron kwa kujitolea kanuni zake kwa "kujipenda" kutokana na mlipuko wa bei ya nishati inayohusishwa na vita.

Ilikuwa ni ziara ya kwanza nchini Ufaransa kwa "MBS" tangu kuuawa nchini Uturuki mnamo 2018 kwa mwandishi wa habari wa Saudi Jamal Khashoggi, mauaji ambayo yalilaniwa na kumhusisha mwanamfalme huyo kuhusika na mauaji hayo, lakini alikanusha yote hayo.

Vita vya Ukraine na mkutano wa kilele wa Paris kwenye menyu

Mbali na uhusiano baina ya nchi hizo mbili, watu hao wawili watajadili "hasa ​​vita vya Ukraine na athari zake kwa ulimwengu mwzima", ilibainisha ikulu ya Elysée.

Emmanuel Macron anasema anataka kuzishawishi nchi zisizofungamana na upande wowote kuweka shinikizo kwa Moscow kukomesha uvamizi wake nchini Ukraine. 

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.