Pata taarifa kuu
UTURUKI- SYRIA-JANGA

UN yaomba msaada kuisaidia Syria

NAIROBI – Umoja wa Mataifa unaomba msaada wa Dola Milioni 397 kuwasaidia, raia wa Syria waliothirika na janga la tetemeko la ardhi, lililosbabisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha maelfu wakihitaji misaada ya kibinadamu.

Malori yaliobeba misaada ya Umoja wa Mataifa yamewasili nchini Syria
Malori yaliobeba misaada ya Umoja wa Mataifa yamewasili nchini Syria AP - Hussein Malla
Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres, ni Katibu Mkuu wa UN.

“Natangaza kuwa Umoja wa mataifa unazindua ombi la kutafuta msaada wa Dola milioni 397 kwa ajili ya masuala ya kibindamu kwa raia wa Syria.” amesema Antonio Guterres, ni Katibu Mkuu wa UN.

Katika hatua nyingine, misaada hasa ya chakula imeanza kuwasili katika eneo linalodhibitiwa na waasi Kaskazini Magharibi mwa Syria baada ya mpaka huo kufunguliwa.

Huko Uturuki, matumaini yameanza kudidimia ya kuwapa hai watu waliofunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.