UN : Watoto milioni 7 Syria, Uturuki wanahitaji msaada
NAIROBI – Shirika la afya duniani, WHO, linasema tetemeko la ardhi lililoikumba nchi ya Uturuki na Syria wiki iliyopita, ni baya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwenye ukanda wa Ulaya katika kipindi cha zaidi ya miaka 100.
Imechapishwa:
Cheza - 00:40
Kauli ya WHO imekuja saa chache tangu ujumbe wa kwanza wa umoja wa Mataifa, ufanikiwe kufika kwenye mji unaokaliwa na waasi, Aleppo, wakati huu taasisi hiyo ikikosolewa kwa kasi ndogo kuwasaidia waathirika wa tetemeko.
Hans Kluge, ni mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya.
“Huu ni muda wa jamii ya kimataifa kuonyesha utu wake kwa nchi ya Uturuki kama ambavyo Uturuki imekuwa ikionyesha kwa mataifa mengine.” ameeleza Hans Kluge
Katika hatua nyingine, shirika la umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF, limesema watoto zaidi ya milioni 7 wanahitaji msaada kufuatia madhara ya tetemeko hilo.