Pata taarifa kuu
UTURUKI/SYRIA - TETEMEKO LA ARDHI

Erdogan amekiri 'mapungufu' katika kukabiliana na tetemeko la ardhi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ametembelea eneo kulikotokea tetemeko la ardhi, huku idadi ya watu waliopoteza maisha ikiongezeka na kufikia zaidi ya Elfu 11 katika nchi hiyo na Syria.

Rais wa Uturuki, Recep Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Erdogan © Burhan Ozbili / AP
Matangazo ya kibiashara

Akizuru eneo hilo, Erdogan amejibu moja kwa moja kuhusu shutuma kwamba serikali yake imeshindwa kutoa idadi ya kutosha ya waokoaji na misaada, huku kukiwa na hasira kubwa kutoka kwa raia kuhusu maandalizi ya serikali kushughulikia janga hili.

Bila shaka, kuna mapungufu, masharti yanaonekana wazi, haiwezekani kuwa tayari kwa janga kama hili," amesema Erdogan.

Nchini Uturuki, karibu watu elfu saba wamepoteza maisha, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda idadi hiyo itaendelea kuongezeka, raia wa maeneo yaliyoathirika  wakilalamikia watalaam wa uokoaji kuchukua muda mrefu.

Mataifa hayo mawili, yameendelea kutoa wito wa msaada wa Kimataifa kuwasaidia watu na kutafuta miili zaidi iliyokwama kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.

EU misaada

Siku ya Jumatano, Umoja wa Ulaya ilithibitisha kutuma msaada wa dola milioni 3.1 kwa Syria, tangazo ambalo linakuja baada ya nchi hiyo kuomba msaada rasmi, chini ya mpango ulioundwa kusaidia nchi zilizokumbwa na janga, kwa kuwezesha Utaratibu wa ulinzi wa raia wa EU.

Kadhalika, EU imetuma msaada wa awali wa dola milioni 2.7 kwa Uturuki.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.