Pata taarifa kuu
ISRAEL-PALESTINE

Mpalestina awajeruhi watu wawili Mashariki mwa mji wa Jerusalem kwa kuwapiga risasi

Mkaazi wa eneo la Mashariki mwa Jerusalem, amewapiga risasi na kuwajeruhi watu wawili katika shambulizi jipya, saa chache baada ya raia wa Palestina kuwauwa watu saba kwa kuwapiga risasi nje ya Sinagogi katika êneo hilo hapo jana.

Maafisa wa usalama, Mashariki mwa Jerusalem
Maafisa wa usalama, Mashariki mwa Jerusalem AP - Mahmoud Illean
Matangazo ya kibiashara

Polisi wa Israel wamesema aliyehusikana na tukio hilo ni kijana mwenye umri wa miaka 13 ambaye hata hivyo, alidhibitiwa na kujeruhiwa. 

Hii imekuja siku moja baada ya  jeshi la Israeli kutekeleza operesheni, katika ukingo wa Magharibi na kuwauwa Wapalestina tisa, huku kundi lenye silaha kwenye ukingo wa Gaza, likirusha makombora katika ardhi ya Israeli. 

Jana usiku, raia wa Palestina, aliyekuwa amejihami kwa bastola, alikwenda mjini Jerusalem na kuwafwatulia risasi watu waliokuwa kwenye ibada ya Kiyahudun na kusababisha saba kupoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa. 

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, amesema serikali yake itachukua hatua baada ya mauaji hayo, wakati huu Umoja wa Ulaya, ikihofia kuwa huenda machafuko zaidi yakashuhudiwa katika ukanda wa Magharibi na kuitaka Israel kutumia nguvu kama hatua  ya mwisho. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.