Pata taarifa kuu
ISRAELI- SIASA

Israel:Netanyahu anarejea madarakani kuongoza Israeli kwa miaka mitano

Benjamin Netanyahu, anarejea tena kama Waziri Mkuu wa Israeli baada ya kufanikiwa kuunda serikali.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israeli
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israeli AP - Maya Alleruzzo
Matangazo ya kibiashara

Netanyahu, mwenye umri wa miaka 73, anakuwa Waziri Mkuu wa muda mrefu nchini humo baada ya kuingia madaraka tangu mwaka 1996 hadi 1999 na baadaye, 2009 hadi 2021.

Nini kitarajiwe, kutoka kwa Netanyahu?

Dokta Brian Wanyama ni mchambuzi wa siasa za Kimataifa akiwa mjini Bungoma nchini Kenya.

“Raia wa Israeli wamempa nafasi ya pili, ya tatu na hata ya nne kuweza kuongoza taifa hilo na kumaanisha ya kwamba wanaimani katika utawala wake.” amesema Dkt Brian Wanyama.

Kinachosubiriwa sasa ni kuona jinsi ambavyo Netanyahu ataongoza taifa wakati huu dunia inapokabiliwa na kipindi kigumu cha uchumi na  athari za Uviko 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.