Mpalestina 1 auawa na 16 wajeruhiwa katika Ukingo wa Magharibi
Mpalestina mmoja ameuawa na wengine 16 kujeruhiwa wakati wa operesheni ya jeshi la Israel mapema Jumanne (Septemba 6) huko Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Imechapishwa:
Operesheni ambayo imelenga kuharibu makazi ya mhusika wa shambulio baya la hivi karibni huko Tel Aviv, imetangaza Wizara ya Afya ya Palestina, ikinukuliwa na shirika la habari la AFP.
"Mhanga mmoja mwenye umri wa miaka 29 na watu 16 wamejeruhiwa kwa risasi au milipuko kutokana na uvamizi wa Israel dhidi ya Jenin," wizara ya Palestina imesema katika ujumbe mfupi kwa vyombo vya habari.
Wakati wa usiku, jeshi la Israeli lilibaini kwamba lilifanya operesheni huko Jenin ili kuharibu makazi ya mhusika wa shambulio ambalo liliua watu watatu mnamo Aprili 7 katikati mwa mji wa Tel Aviv.