Pata taarifa kuu

Israel na Uturuki zarejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka 12

Israel na Uturuki zimetangaza leo Jumatano kurejeshwa kamili kwa mahusiano yao ya kidiplomasia, ambayo yamedorora tangu meli ya Mavi Marmara, iliyovamiwa na majeshi ya Israel mwaka 2010. Lakini Ankara imethibitisha nia yake ya "kuendelea kuwatetea" Wapalestina.

در ماه مارس ۲٠۲۲ اسحاق هرتزوگ رئیس جمهوری اسرائیل با همتای ترک خود اردوغان دیدار کرد
در ماه مارس ۲٠۲۲ اسحاق هرتزوگ رئیس جمهوری اسرائیل با همتای ترک خود اردوغان دیدار کرد AP - Burhan Ozbilici
Matangazo ya kibiashara

Ukurasa wa kidiplomasia umefunguliwa kwa vigogo hawa wawili ambao wamekuwa kimya kwa miaka kumi na miwili. Israel imetangaza Jumatano Agosti 17 kurejeshwa kamili kwa uhusiano wa kidiplomasia na Uturuki na kurejea kwa mabalozi katika nchi zote mbili.

"Iliamuliwa kuongeza kiwango cha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa uhusiano kamili wa kidiplomasia na kurejesha mabalozi katika nchi hizo mbili," Waziri Mkuu wa Israeli Yair Lapid amesema katika taarifa.

"Kurejeshwa kwa uhusiano na Uturuki ni hatua muhimu kwa utulivu wa kikanda na habari muhimu sana za kiuchumi kwa raia wa Israeli," ameongeza.

Mjini Ankara, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu amebainisha kwamba Uturuki "haitoacha kuitetea Palestina".

Uhusiano wa pande mbili kati ya Israel na Ankara ulidorora mwaka wa 2010 na kadhia ya meli ya Mavi Marmara, wakati majeshi ya Israel yalipoanzisha mashambulizi mabaya kwenye meli hii ya Uturuki ikijaribu kupeleka msaada katika Ukanda wa Gaza, eneo la Wapalestina linalokabiliwa na marufu ya Israel. Nchi hizo mbili ziliwaita mabalozi wao mnamo mwaka wa 2018 baada ya vifo vya waandamanaji wa Kipalestina huko Gaza.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mtetezi mkubwa wa haki ya Palestina, mara nyingi amekosoa sera za Israel dhidi ya Wapalestina.

Israel na Uturuki hivi majuzi zilikaribisha mabadiliko katika mahusiano yao, hasa ziara ya Rais Isaac Herzog mwezi Machi nchini Uturuki, ikiwa ni ziara ya kwanza ya mkuu wa taifa la Israel tangu mwaka 2007 nchini humo. Mkuu wa diplomasia ya Uturuki alifanya ziara mjini Jerusalem mwishoni mwa mwezi Mei kama sehemu ya suluhu hii ya kidiplomasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.