Pata taarifa kuu

Afghanistan: Makumi ya watu wafariki dunia kufuatia tetemeko kubwa la ardhi

Takriban watu 300 wameuawa kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea karibu na mji wa Khost kusini mashariki mwa Afghanistan, karibu kabisa na mpaka na Pakistan. Mamlaka inahofia kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Tetemeko la ardhi limetokea karibu na mji wa Khost, kusini-mashariki mwa Afghanistan, karibu sana na mpaka na Pakistan.
Tetemeko la ardhi limetokea karibu na mji wa Khost, kusini-mashariki mwa Afghanistan, karibu sana na mpaka na Pakistan. RFI
Matangazo ya kibiashara

Juhudi za kuwasiliana na wakazi ambao wako katika eneo la tukio hazijafaulu kuutokana na kuwa mtandao wa simu haufanyi kazi, kufikia sasa bado hali ni nzito.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.9 katika kipimo cha Richter limesikika katika zeneo hilo lakini pia kilomita kadhaa kutoka kwenye kitovu, hadi sasa huko Islamabad wengi hawajasikia tetemeko hilo. Kitovu cha tetemeko hilo kinapatikana kilomita 400 kutoka mji mkuu wa Afghanisatan, Islamabad, kusini mashariki mwa Afghanistan.

Mamlaka yatoa wito kwa usaidizi

Eneo lililoathiriwa ni la milima na katika vijiji, ambapo nyumba hujengwa kwa udongo, hali ambayo haistahamili matetemeko ya ardhi ambayo hutokea mara kwa mara nchini Afghanistan, hasa katika eneo la milima ya Hindu Kush linalopatikana kwenye makutano kati ya bamba za tectonic za Eurasia na India.

Mwezi wa Januari mwaka huu, eneo la magharibi mwa Afghanistan lilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.3 katika kipimo cha Richter; Watu 26 waliuawa. Mamlaka ya Afghanistan inaomba msaada kuwaokoa wakaazi waliokwama kwenye vifusi vya nyumba zao. Inafahamika kwamba uwezo wa utawala wa Taliban ni mdogo. Afghanistan inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu wakati nchi hiyo, ambayo ilikuwa ikiishi kwa kuongezewa misaada ya kimataifa, iliona misaada hiyo ikikatwa baada ya Taliban kuchukua madaraka mwezi wa Agosti mwaka uliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.