Pata taarifa kuu

UN: Baraza la usalama limekashifu mauwaji ya mwanahabari wa Al Jazeera.

Braza la usalama katika umoja wa mataifa kwa pamoja limekashifu mauawaji ya mwanahabari Shireen Abu Akleh, mwenye asili ya Palestina na Marekani, UN ikitaka uchunguzi huru na wa haraka kufanyika kubaini kilichotokea.

Polisi wa Israeli wakikabiliana na wapalestina wakati wa mazishi ya mwanahabari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh.
Polisi wa Israeli wakikabiliana na wapalestina wakati wa mazishi ya mwanahabari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh. © Maya Levin - AP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya UN imekuja saa chache baada ya maofisa wa polisi wa Israeli kuonekeana wakiwapiga wamombolezaji wakati wa mazishi ya mwanahabari huyo jijini  Jerusalem.

Abu Akleh, aliyekuwa anafanya kazi na shirika la habari la Al Jazeera, aliuawa wakati akifuatilia makabiliano katika kambi ya wakimbizi ya Jenin kwenye eneo la ukingo wa magharibi.

Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas ambaye ameishtumu Israel kwa kuhusika na mauaji ya mwanahabari huyo,ametaka Israeli kuwajibishwa taarifa zikidai kuwa aliauwa na wanajeshi wa Israeli.

Mauaji yake, yamezua mvutano kati ya Palestina na Israeli, huku kila mmoja akimlaumu mwenzake. Kituo cha Aljazeera, kimesisistiza mwanahabri wake, alipigwa risasi kwa makusudi.

Uchunguzi wa awali wa Israel unaonesha kuwa, ni vigumu kufahamu ni nani hasa aliyehusika na mauaji ya mwanahabari huyo kwa kumpiga risasi.

Palestina ilikataa kushirikiana na Israeli kuchunguza mauaji hayo, huku Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa ukitaka ukweli kuwekwa wazi na wahusika kuchukuliwa hatua.

Mauawaji yake yamelaaniwa vikali kote duniani wakati huu mataifa ya Israeli na Palestina yakituhumiana kuhusu ni nani aliyehusika na kitendo hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.