Pata taarifa kuu

Uturuki yaanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya PKK kaskazini mwa Iraq

Operesheni hiyo inayolenga maeneo matatu karibu na mpaka wa Uturuki,  inahusisha vikosi maalum na ndege zisizo na rubani. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi, mashambulizi hayo yanalenga kuzuia mashambulizi makubwa ya PKK dhidi ya Uturuki. Lakini Ankara inatafuta zaidi ya yote kudhoofisha uanzishwaji wa kijeshi kwa wapiganaji wa Kikurdi katika maeneo haya.

Mwanajeshi akiwa ameshikilia bunduki kwenye gari linaloshiriki katika doria ya pamoja ya Urusi na Uturuki katika mashamba ya mji wa al-Jawadiyah wa Syria kaskazini mashariki mwa mkoa wa Hasakeh karibu na mpaka na Uturuki, Disemba 24, 2020.
Mwanajeshi akiwa ameshikilia bunduki kwenye gari linaloshiriki katika doria ya pamoja ya Urusi na Uturuki katika mashamba ya mji wa al-Jawadiyah wa Syria kaskazini mashariki mwa mkoa wa Hasakeh karibu na mpaka na Uturuki, Disemba 24, 2020. AFP - DELIL SOULEIMAN
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii mpya ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Uturuki tangu mwezi Mei 2019 katika maeneo haya ya kaskazini mwa Iraq ambapo PKK inakabiliana na vikosi vya serikali ya Mkoa wa Kurdistan.

Shambulio hilo pia linakuja siku mbili baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa Kurdistan ya Iraq, Masrour Barzani nchini Uturuki, ambaye bila shaka Recep Tayyip Erdogan alikuwa amemjulisha.

Mamlaka ya Ankara, ambayo inajivunia kuwa imedhoofisha PKK nchini Uturuki hata katika miaka ya hivi karibuni, sasa inaelekeza mashambulizi yao kwenye kambi kuu za kijeshi za kundi la Wakurdi nchini Iraq, hasa katika maeneo ya milimani ya Gara na Zap. Operesheni hiyo iko hatarini, kwa sababu ya uwepo wa wanajeshi wa Uturuki kwenye uwanja huu ambao PKK wanaujua vyema, baada ya kuwepo kwa miongo kadhaa.

Mashambulizi ya jeshi la Uturuki yameongeza mvutano kati ya Ankara na serikali kuu ya Iraq huko Baghdad. Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar amesema operesheni hiyo inaheshimu "uadilifu wa eneo na mamlaka ya Iraq, nchi yenye urafiki na udugu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.