Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA

Saudia kufungua tena mipaka yake kwa mahujaji waliopewa chanjo dhidi ya Covid-19

Saudi Arabia itafungua tena hija ya Omra (hija ndogo) kwenda Makka kwa mahujaji kutoka nchi za kigeni waliopewa chanjo dhidi ya Covid-19, shirika la habari la Saudi Arabia limeripoti Jumapili (Agosti 8).

Janga la Covid-19 limevuruga sana ibada ya Hija na Umrah, vyanzo muhimu vya mapato kwa nchi hii ya kifalme ambavyo huingiza dola bilioni 12 kwa mwaka.
Janga la Covid-19 limevuruga sana ibada ya Hija na Umrah, vyanzo muhimu vya mapato kwa nchi hii ya kifalme ambavyo huingiza dola bilioni 12 kwa mwaka. © REUTERS - Ahmed Yosri
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya Saudia itaanza kuidhinisha maombi ya kuingia nchini humo kuanzia kesho Jumatatu, shirika hilo limesema. Mipaka ya nchi hiyo ilifungwa miezi 18 iliyopita kutokana na janga hilo hatari.

Hija ndogo (Umrah), ambayo ni tofauti na Hija kubwa, inaweza kufanywa kwa mwaka mzima, kawaida huvutia mamilioni ya wageni kutoka kote ulimwenguni kila mwaka.

Janga la Covid-19 limevuruga sana ibada ya Hija na Umrah, vyanzo muhimu vya mapato kwa nchi hii ya kifalme ambavyo huingiza dola bilioni 12 kwa mwaka.

Riyadh yataka kufufua utalii

Hadi sasa, ni mahujaji waliopewa chanjo tu wanaoishi Saudi Arabia ndio walioikubaliwa kufanya Hija ndogo (Umrah).

Mahujaji wa kigeni wanaotaka kusafiri kwenda Makka pia watahitaji kupatiwa chanjo, na kibali kinachotambuliwa na Saudi Arabia, na kuzingatia sheria za karantini, shirika la habari la Saudi limeongeza, likinukuu wizara yenye dhamana ya Hija.

Saudi Arabia imewekeza mabilioni katika tasnia ya utalii katika miaka ya hivi karibuni ili kubadilisha uchumi wake wa mafuta. Kwa muda mrefu, nchi hii ilitoa visa vya kwanza vya watalii mwaka 2019. Kati ya mwezi Septemba 2019 na kufungwa kwa mipaka mwezi Machi 2020, ilitoa visa 400,000 za watalii.

Tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya, Saudi Arabia imerekodi zaidi ya visa 5,321,000 vya maambukizi na zaidi ya vifo 8,300.

Serikali iliharakisha kampeni ya chanjo mapema Agosti, kwa lengo la kufufua utalii na kuandaa hafla za michezo na maonyesho.

Chanjo sasa ni lazima kuingia katika vituo vya umma na vya kibinafsi, pamoja na shule na maeneo ya burudani, na pia kutumia usafiri wa umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.