Pata taarifa kuu
LIBAN-UCHUMI

Mlipuko wa bandari ya Beirut: Macron aandaa kuchangisha fedha kwa Lebanon

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atajaribu kukusanya zaidi ya dola milioni 350 (euro milioni 295) kusaidia Lebanon wakati wa mkutano ulioandaliwa kusaidia raia wa Lebanon, mwaka mmoja baada ya mlipuko wa bandari ya Beirut.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akichunguza bandari ya Beirut iliyoharibiwa na mlipuko Agosti 6, 2020, siku mbili baada ya mlipuko huo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akichunguza bandari ya Beirut iliyoharibiwa na mlipuko Agosti 6, 2020, siku mbili baada ya mlipuko huo. Thibault Camus/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mwaka mmoja baada ya mlipuko ulioharibu bandari ya mji mkuu na kuitumbukiza Lebanon katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi, viongozi wake wa kisiasa bado wameshindwa kuunda serikali, licha ya shinikizo la Ufaransa na kimataifa.

"Kadiri hali inavyoendelea kuzorota, hitaji la serikali linazidi kuwa la haraka zaidi," mshauri wa Emmanuel Macron amewaambia waandishi wa habari.

Ufaransa imeongoza juhudi za kimataifa ili kuiondoa koloni lake la zamani katika mgogoro huo. Emmanuel Macron ambaye amezuru mji wa Beirut mara mbili tangu kutokea kwa mlipuko huo, alitoa msaada wa dharura na kuchukua hatua za kuzuia kuingia nchini Ufaransa maafisa wa Lebanon ili nchi hiyo iweze kuweka mpango wa mageuzi.

Ameshawishi pia Umoja wa Ulaya kukubaliana juu ya mfumo wa vikwazo ulio tayari kutumika.

Lakini mipango yake, ikiwa ni pamoja na kupata ahadi kutoka kwa wanasiasa wa Lebanon kukubaliana juu ya kuwekwa kwa serikali ya mageuzi, bado haijafanikiwa.

Rais wa Marekani Joe Biden atahudhuria mkutano huo, ambao unaandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, ofisi ya rais wa Ufaransa imesema, Viongozi 40 duniani, ikiwa ni pamoja na rais wa Misri, kiongozi wa Jordan, Iraq na Canada  watashiriki mkutano huo. Uingereza itawakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya nje.

Mwaka jana, mkutano uliofanyika baada ya mlipuko ulikusanya karibu dola milioni 280.

Msaada huo mpya wa kibinadamu hautakuwa na masharti yoyote, ofisi ya Emmanuel Macron imesema, lakini karibu dola bilioni 11 zilizokusanywa mwaka 2018 bado zinazuiliwa kwa masharti ya mageuzi kadhaa yatakayotekelezwa na viongozi wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.