Pata taarifa kuu
IRAN - UCHAGUZI

Wananchi wa Iran wajitokeza kwa wingi kupiga kura kumchaguwa rais

Raia wa Iran wanapiga kura, kumchagua rais katika uchaguzi ambao umekumbwa na wengi wa  wagombea kuondolewa kwenye kinyanganyiro hicho.

Mchanganyiko huu wa picha nne unaonyesha wagombea wa uchaguzi wa urais wa Irani Juni 18, 2021 kutoka kushoto kwenda kulia; Abdolnasser Hemmati, Mohsen Rezaei, Amir Hossein Ghazizadeh Hashemi na Ebrahim Raisi. Wairani watapiga kura Ijumaa juu ya nani anapaswa kuwa rais ajaye wa nchi hiyo wakati wa mvutano na Magharibi juu ya makubaliano yake ya nyuklia yaliyochakaa na nguvu za ulimwengu.
Mchanganyiko huu wa picha nne unaonyesha wagombea wa uchaguzi wa urais wa Irani Juni 18, 2021 kutoka kushoto kwenda kulia; Abdolnasser Hemmati, Mohsen Rezaei, Amir Hossein Ghazizadeh Hashemi na Ebrahim Raisi. Wairani watapiga kura Ijumaa juu ya nani anapaswa kuwa rais ajaye wa nchi hiyo wakati wa mvutano na Magharibi juu ya makubaliano yake ya nyuklia yaliyochakaa na nguvu za ulimwengu. AP
Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi wa 13 wa urais nchini Iran, chini ya katiba ya nchi hiyo.

Wagombea wanne, wanatafuta uongozi wa nchi hiyo inayopatika Magharibi mwa barra Asia.

Rais Hassan Rouhani hawanii tena, kwa sababu tayari amehudumu kwa mihula miwili, na anaondoka madarakani baada ya miaka minane.

Kati ya wagombea hgao wanne, Mhubiri wa dini ya Kiislamu Ebrahim Raisi ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi.

Kiongozi wa juu nchini humo Ayatollah Ali Khamenei, tayari amepiga kura yake jijini Tehran na kutoa wito kwa wapiga kura Milioni 60 kujitokeza kwa wingi.

Vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kufungwa kufikia saa sita siku ya Ijumaa, huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa siku ya Jumamos, katika taifa hilo ambalo limeendelea kuwekewa vikwazo vya kiuchumli na Marekani kutokana na madai ya kuendeleza mradi wa nyuklia kwa lengo la kutengeza silaha za maangamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.