Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Serikali ya Afghanistan na Taliban wakutana tena kwa mazungumzo Doha

Serikali ya Afghanistan na Taliban wameanza tena mazungumzo huko Doha tangu Jumanne wiki hii kujadili mchakato wa amani wa Afghanistan, mkutano wao wa kwanza tangukusindwa kwa  majaribio la mazungumzo mapema mwaka huu.

Mazungumzo ambayo yalianza Doha mwezi wa Septemba uliyopita kumaliza miongo kadhaa ya vita yamekwama baada ya vikao vichache vya mazungumzo na vurugu nchini Afghanistan zimezidi kuongezeka tangu Marekani ilipoanza kuondoa wanajeshi wake.
Mazungumzo ambayo yalianza Doha mwezi wa Septemba uliyopita kumaliza miongo kadhaa ya vita yamekwama baada ya vikao vichache vya mazungumzo na vurugu nchini Afghanistan zimezidi kuongezeka tangu Marekani ilipoanza kuondoa wanajeshi wake. © AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Taliban Suhail Shaheen amethibitisha kwenye mtandao wa Twitter Jumatano kwamba wakuu wa ujumbe kutoka pande zotembili, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wajumbe wao, walikuwa wawameanza tena mazungumzo siku moja kabla katika mji mkuu wa Qatar.

"Walijadili mada kwenye zilizokuwa zimewekwa kwenye ajenda, kuendeleza kwa kasi mchakato wa mazungumzo," alisema.

Mkutano huo ulikuwa mkutano wa kwanza rasmi kati ya pande hizo mbili tangu katikati ya mwezi Mei baada ya kufutwa mwezi Aprili, kufuatia hatua ya Marekani kutangaza kuwa itaondoa majeshi yake ifikapo Septemba 11, mazungumzo ya hapo awali yalikuwa yameanza vibaya.

Mazungumzo ambayo yalianza Doha mwezi Septemba uliyopita kumaliza miongo kadhaa ya vita yamekwama baada ya vikao vichache vya mazungumzo na vurugu nchini Afghanistan zimezidi kuongezeka tangu Marekani ilipoanza kuondoa wanajeshi wake.

Kipaumbele cha juu kwa nchi za Magharibi, na haswa Merika, ni kupata maelewano kati ya pande mbili zinazokinzana.

Waziri Mkuu wa Pakistani Imran Khan alisema wiki iliyopita kwamba nchi yake ilikuwa ikishinikiza suluhu ya kisiasa nchini Afghanistan kabla ya kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni, ili kupunguza hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.