Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Afghanistan: Kumi na moja wauawa katika mlipuko wa bomu

Takriban watu kumi na moja wameuawa nchini Afghanistan katika mlipuko wa bomu dhidi ya basi, saa chache kabla ya kundi la Taliban kutangaza kusitisha mapigano kwa siku tatu kwa ajili ya Eid al-Fitr, Wizara ya Mambo ya Ndani imetangaza Jumatatu Mei 10.

Mazishi ya watu wengi yakifanyika kwa pamoja katika makaburi ya huko Kabul, Mei 9, 2021.
Mazishi ya watu wengi yakifanyika kwa pamoja katika makaburi ya huko Kabul, Mei 9, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili, ambalo pia limejeruhi watu 28, lilitokea usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu katika mkoa wa Zabul, kusini mashariki mwa nchi, Tareq Arian, msemaji wa wizara hiyo, amewaambia waandishi wa habari, akinukuliwa na shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo, mazishi ya watu waliouawa mwishoni mwa wiki iliyopita kufuatia shambulizi la bomu nje ya shule moja ya sekondari katika jiji kuu Kabul yanafanyika.

Watu 60 waliuawa katika shambulizi hilo, wengi wakiwa ni wanafunzi, wasichana.

Mpaka sasa hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, katika eneo ambalo limekuwa likilengwa na kundi la kigaidi la Kisunni.

Taliban yazidi kunyooshewa kidole cha lawama

Hata hivyo, serikali ya Afganistan imewalaumu wapiganaji wa Taliban kwa kuhusika na shambulizi hilo ambamlo hata hivyo wamekanusha.

Mwaka mmoja uliopita katika eneo hilo, kulitokea na shambulizi kama hili katika hospitali ya wanawake kujifungua na kusababisha vifo vya wanawake 24 na watoto wachanga.

Lengo la shambulizi la mwishoni mwa juma lililopita, halijafahamika lakini nchi hiyo imeanza tena kushuhudia ongezeko la mashambulizi wakati huu Marekani inapojiandaa kuwaondoa wanajeshi wake wote nchini humo ifikapo tarehe 11 mwezi Septemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.