Pata taarifa kuu
ISRAELI

Israeli yafuta sharti la uvaaji barakoa

Israeli imechukua uamuzi wa kufuta sharti la watu kuvaa barakoa wakiwa nje ya makwao na kufungua shule zote, hatua ya mwisho kuelekea kurudi kwa maisha ya kawaida kutokana na kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya janga la orona iliyofanywa nchini

Watu wanatembea barabarani katika jiji la pwani la Israeli la Tel Aviv baada ya mamlaka kutangaza kwamba imefuta sharti la uvaaji barakoa kuzuia COVID-19.
Watu wanatembea barabarani katika jiji la pwani la Israeli la Tel Aviv baada ya mamlaka kutangaza kwamba imefuta sharti la uvaaji barakoa kuzuia COVID-19. JACK GUEZ AFP
Matangazo ya kibiashara

Israeli imeshuhudiwa kupungua kwa kasi kwa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19, na karibu 54% ya idadi ya watu milioni 9.3 wamechomwa sindano mbili za chanjo ya Pfizer / BioNTech.

Sharti la kuvaa barakoa, hatua iliyokuwa chini ya idara ya polisi na kuamriwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, limefutwa Jumapili hii, lakini wizara ya afya imeeleza kwamba bado shati hili  linahitajika katika nafasi za umma za ndani, ikiwataka raia kila wakati kuwa na barakoa karibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.