Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI

Jean Arnault ateuliwa kuwa mjumbe maalum wa UN Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua Mfaransa Jean Arnault kuwa mjumbe wake nchini Afghanistan

Uteuzi wa Jean Arnault "unaonyesha juhudi za Umoja wa Mataifa katika utatuzi wa amani wa mzozo nchini Afghanistan," amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.
Uteuzi wa Jean Arnault "unaonyesha juhudi za Umoja wa Mataifa katika utatuzi wa amani wa mzozo nchini Afghanistan," amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, msemaji wa Umoja wa Mataifa amebaini kwamba Antonio Guterres amemtaka Jean Arnault kumwakilisha katika hitimisho la suluhu la kisiasa la mgogoro nchini humo, akishirikiana bega kwa bega na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNAMA) unaoongozwa na raia wa Canada Deborah Lyons na washirika wa kikanda.

Jean Arnault alikuwa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia.

Atachukua jukumu kuu katika mazungumzo ya amani ambayo yametangazwa wiki hii huko Moscow. Mwanadiplomasia huyo wa Ufaransa ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa mwakilishi maalum kwa Afghanistan na eneo jirani.

Uteuzi wa mwanadiplomasia huyo wa Ufaransa "unaonyesha juhudi za Umoja wa Mataifa katika utatuzi wa amani wa mzozo nchini Afghanistan," amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.

Uteuzi wa mtu kutoka Ulaya kwa wadhifa wa mjumbe maalum wa  Umoja wa Mataifakwa Afghanistan unakuja siku moja baada ya kuanzishwa kwa mazungumzo huko Moscow, ambayo yanalenga kutoa mwelekeo mpya katika mchakato wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.