Pata taarifa kuu
IRAQ-VATICAN-DINI-USHIRIKIANO

Ziara ya Papa nchini Iraq: Ziara yenye hatari kubwa kwa nchi isiyo na utulivu

Kiongozi wa kanisa Katolika duniani Papa Francis anaanza ziara ya kihistoria nchini Iraq leo Ijumaa. Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa kanisa Katoloki kuzuru nchi hii, ambapo changamoto ni kubwa na hali ya usalama ni tete.

Mabango mengi yaliyoandikwa kwa maneno ya Kiarabu na Kiingereza kumkaribisha Papa Francis yakitundikwa huko Baghdad kabla ya kuwasili kwa kwake.
Mabango mengi yaliyoandikwa kwa maneno ya Kiarabu na Kiingereza kumkaribisha Papa Francis yakitundikwa huko Baghdad kabla ya kuwasili kwa kwake. REUTERS - KHALID AL-MOUSILY
Matangazo ya kibiashara

Safari hii itadumu siku tatu, wakati ambapo kiongozi huyo wa kanisa Katolika duniani atatembelea miji ya Baghdad, Najaf na Ur kusini mwa nchi, kisha Erbil, Qaraqosh na Mosul kaskazini.

Papa Francis amesisitiza kufanya ziara hiyo licha ya ongezeko jipya la maambukizi ya virudsi vya COVID-19 nchini Iraq na hofu dhidi ya usalama wake.

Papa atakutana na kiongozi wa Waislamu wa dhehebu la Kishia anayeheshimiwa sana, na kufanya sala huko Mosul na kuhudhuria misa katika uwanja wa michezo.

Ziara hii ya siku nne inakusudiwa kuihakikishia jamii ya Kikristo nchini Iraq inayopungua kwa kasi kubwa na kukuza mazungumzo kati ya dini.

Papa Francis analenga kuwatia mayo Wakristo wanaoteswa na kushinikiza amani katika mikutano na viongozi wa kisiasa na kidini.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.