Pata taarifa kuu
SAUDIA-MAREKANI-HAKI-USALAMA

Saudia yakanusha madai ya kumhusisha Bin Salman na kifo cha Khashoggi

Saudi Arabia imefutlia mbali madai ya kumhusisha kumhusisha Bin Salman na kifo cha Khashoggi yalitolewa katika ripoti ya kijasusi iliyotolewa na Marekani ikifichua kuwa Mwana mfalme huyo aliidhinisha mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi mwaka 2018.

Jamal Khashoggi, hapa ilikuwa mwaka 2014, aliuawa katika ubalozi mdogo wa Istanbul, Uturuki Oktoba 2018.
Jamal Khashoggi, hapa ilikuwa mwaka 2014, aliuawa katika ubalozi mdogo wa Istanbul, Uturuki Oktoba 2018. MOHAMMED AL-SHAIKH AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia imesema inaipinga vikali ripoti hiyo ikisema imejaa taarifa za uzushi.

"Tumefikia hitimisho kwamba mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman aliidhinisha operesheni ya kumkamata au kumuua mwandishi wa habari wa Saudi Jamal Khashoggi huko Istanbul, nchini Uturuki," idara ya kitaifa ya pelelezi iliandika katika waraka mfupi wa kurasa nne.

"Mohammed bin Salman alimchukulia  Khashoggi kama tishio kwa utawala wa kifalme na kwa upana aliunga mkono utumiaji wa hatua kali ikiwa ni lazima kumnyamazisha," imeongeza idaya yakitaifa ya upelelezi ya Marekani.

Ripoti hiyo inabaini kwamba mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salmani alikuwa na "udhibiti kamili" wa idara za ujasusi na usalama wa nchi hiyo ya kifalme tangu mwaka 2017."

Idara za ujasusi nchini Marekani pia zinadhani kwamba, wakati wa kuuawa kwa Jamal Khashoggi, Mohammed ben Salman aliweka mazingira ambayo washirika wake labda wasingeweza thubutu kuweka hatarini maagizo waliopewa, "kwa kuogopa" kufukuzwa au kukamatwa ".

Hapo kabla Saudi Arabia ilisema mauaji ya Khashoggi kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia nchini Uturuki yalifanywa katika operesheni ya kihalifu na kukanusha kuhusika kwa mwanamfalme Salman.

Hata hivyo Mohammed bin Salman, ameendelea kukanusha kuhusika na mauaji hayo hata baada ya washauri wake wa karibu kutiwa hatiani na mamlaka za sheria nchini Suadi Arabia.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema Washington inalenga kuchukua mwelekeo mpya wa kisera lakini siyo kuvuruga mahusiano yake na Saudi Arabia ambayo ni mshirika wa karibu wa usalama kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani akiandika ripoti zinazomkosoa Mohammed Salman na serikali ya Saudi Arabia, aliuwawa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2018.

Muandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati wa mauaji yake, aliambiwa na balozi wa Saudia afike katika ubalozi wa taifa hilo mjini Istanbul, ili kupata nyaraka kadhaa alizohitaji ili aweze kufunga ndoa na mpenzi wake raia wa Uturuki, Hatice Cengiz.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.