Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Kabul na Taliban wakubaliana kuhusu masharti ya mazungumzo

Wawakilishi wa serikali ya Afghanistan na Taliban wamefikia makubaliano leo Jumatano kuhusu masharti ya mazungumzo yao ya amani, pande hizo mbili zimesema, kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Kiongozi wa kundi la Taliban, Abdul Ghani Baradar, akiwa na mwakilishi wa serikali ya Marekani na Afghanistan, Zalmay Khalilzad, hapa ilikuwa Doham Qatar katika moja ya mazungumzo
Kiongozi wa kundi la Taliban, Abdul Ghani Baradar, akiwa na mwakilishi wa serikali ya Marekani na Afghanistan, Zalmay Khalilzad, hapa ilikuwa Doham Qatar katika moja ya mazungumzo REUTERS/Ibraheem al Omari
Matangazo ya kibiashara

"Mchakato wa mazungumzo, pamoja na utangulizi, umekamilika na, kuanzia sasa, mazungumzo yatajikita kuhusu (maswala) ya ajenda," Nader Nadery, mmoja wa wajumbe wa serikali, ameliambia shirika la habari la REUTERS.

 

Msemaji wa Taliban amethibitisha habari hiyo kwenye mdandao wa kijamii wa Twitter. Haya ni makubaliano ya kwanza yaliyoandikwa kati ya pande hizo mbili katika mchakato ulioanzishwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa.

 

Mazungumzo yalianza mnamo mwezi Septemba huko Doha, nchini Qatar, kulingana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Marekani na Taliban mnamo mwezi Februari, ambayo yanaeleza kuondoka kwa vikosi vya marekani nchini Afghanistan katika kipindi cha miezi 14.

 

"Wanafunzi wa kidini" hata hivyo hawajaweka silaha zao chini na mkataba wa kusitisha vita utakuwa suala muhimu zaidi katika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.