Pata taarifa kuu
ISRAEL-LEBANON-HEZBOLLAH-USALAMA

Israel yashambulia ngome za Hezbollah nchini Lebanon

Jeshi la Israel limetekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon kwa kujibu mashambulizi ya maroketi yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi hilo.

Wanajeshi waisrael wametumia ndege za kivita kwa kurusha makombora na risasi za moto baada ya kurushiwa risasi kutoka upande wa mpakani wa Lebanon, jeshi la Israel limebaini.
Wanajeshi waisrael wametumia ndege za kivita kwa kurusha makombora na risasi za moto baada ya kurushiwa risasi kutoka upande wa mpakani wa Lebanon, jeshi la Israel limebaini. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ndege za Israel zimetekeleza mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la Kishia la Hebollah mapema Jumatano asubuhi baada ya wapiganaji wa kundi hilo wakiwa nchini Lebanon, kuwarushia makombora askari wa Israel, jeshi la Israel limesema katika taarifa.

Hakuna askari wa Israeli aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo, jeshi la Israel limeongeza.

Wanajeshi waisrael wametumia ndege za kivita kwa kurusha makombora na risasi za moto baada ya kurushiwa risasi kutoka upande wa mpakani wa Lebanon, jeshi la Israel limebaini.

"Kwa kujibu mashambulizi ya Hezbollah, helikopta za kushambulia na ndege ya jeshi la Israel, IDF, (Israel Defense Forces) zimetekeleza mashambulizi usiku dhidi ya ngome za kundi la kigaidi la Hezbollah katika eneo la mpakani," jeshi la Israel (Tsahal) limesema katika taarifa.

Hezbollah haijatoa tamko lolote kuhusiana na mashambulizi hayo ya jeshi la Israel.

Hali ya sintofahamu imeongezeka kwenye mpaka kati ya Israeli na Lebanon. Mwezi uliopita, serikali ya Kiyahudi ilimshtumu Hezbollah kwa kujaribu kukuingia katika ardhi ya Israel, madai ambayo kundi hilo linaloungwa mkono na Iran limekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.