Pata taarifa kuu
SUADI ARABIA-KHASHOGGI-HAKI

Watoto wa Khashoggi 'wasamehe' wauaji wa baba yao

Watoto wa mwandishi wa habari wa Saudia Jamal Khashoggi, aliyeuawa mnamo mwezi Oktoba 2018 kwenye ubalozi wa Saudi Arabia katika mji mkuu wa Uturuki, Istanbul, wamesema leo Ijumaa kuwa wamewasamehe wauaji wa baba yao.

Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2, 2018 katika majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul.
Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2, 2018 katika majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul. MOHAMMED AL-SHAIKH / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wakati wa usiku huu mtakatifu wa mwezi huu mtakatifu (wa Ramadhani) tunakumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu aliposema: ikiwa mtu anasamehe na akakubali kupatanishwa, mtu huyo ana ujira mkubwa mbele yake Mwenyezi Mungu," Salah Khashoggi, mtoto wa mwandishi huyo wa habari, ameandika kwenye Twitter.

"Hii ndio sababu sisi, watoto wa marehemu Jamal Khashoggi, tunatangaza kwamba tumewasamehe wale waliomuua baba yetu," ameongeza.

Salah, mtoto wa mwandishi wa habari aliyeuliwa Oktoba 2, alipokelewa katika kasri ya mfalme Saudi Arabia, akisabahiana kwa mikono na Mwanamfalme Mohammed bin Salman, anayeshukiwa kuwa mdhamini wa mauaji ya babake Jamal Khashoggi.
Salah, mtoto wa mwandishi wa habari aliyeuliwa Oktoba 2, alipokelewa katika kasri ya mfalme Saudi Arabia, akisabahiana kwa mikono na Mwanamfalme Mohammed bin Salman, anayeshukiwa kuwa mdhamini wa mauaji ya babake Jamal Khashoggi. Handout / Saudi Press Agency / AFP

Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2, 2018 katika majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia huko Istanbul. Washtakiwa watano walihukumiwa kifo na wengine watatu kufungwa jela baada ya kesi iliyosikilizwa Desemba mwaka jana nchini Suadi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.