Pata taarifa kuu
LEBANON-IMF-UCHUMI

Lebanon yapata mpango dhidi ya mgogoro wa kiuchumi, hatua muhimu kuelekea kupata msaada wa IMF

Lebanon inatarajia kupata msaada kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) baada ya serikali kupitisha muswada wa mageuzi ya kifedha ambayo yataiwezesha kuondokana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi ambao, unaweza kudumu miaka mitano, amesema Waziri Mkuu Hassan Diab.

Libanon yaendelea kukumbwa na hali mbaya ya uchumi.
Libanon yaendelea kukumbwa na hali mbaya ya uchumi. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hali mbaya ya kiuchumi nchini Lebanon, ambapo sarafu yake imepoteza nusu ya thamani yake tangu mwezi Oktoba, ni tishio kubw kwa utulivu wa nchi hii tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1975-1990.

Mapema wiki hii, maandamano dhidi ya kuzorota kwa hali ya maisha yalisababisha kifo cha mmoja huko Tripoli.

"Tutatumia (mpango) huu kupata na fasi ya mazungumzo na IMF," Hassan Diab amewaambia waandishi wa habari.

"Ikiwa tutapata (msaada wa IMF), na Mungu anataka tuupate, utatusaidia kukabiliana na kipindi hiki kigumu cha uchumi, ambacho kinaweza kudumu miaka mitatu, nne au mitano," Hassan Diab amesema na kuongeza kuwa kiasi cha msaada wa IMF itakuwa moja ya masuala yatakayogubika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.