Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA-SIASA

Saudi Arabia yafutilia mbali tangazo la utawala binafsi kwa wanaotaka kujitenga

Mamlaka katika mikoa tano ya kusini mwa taifa la Yemen imekataa pendekezo la kundi la waasi linalotaka eneo hilo kujitenga. Kundi la Southern Transitional Council, STC limesema kwamba litaunda mamlaka huru na kutangaza hali ya dharura kusini mwa nchi hiyo.

Aidarous al-Zoubeidi, mkuu wa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen, Januari 16, 2020 huko Aden.
Aidarous al-Zoubeidi, mkuu wa Baraza la Mpito la Kusini mwa Yemen, Januari 16, 2020 huko Aden. Saleh Al-OBEIDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi la STC ambalo linaungwa mkono na nchi ya Miliki za Kiarabu, limejiondoa kwenye  mkataba wa amani ambao lilitia saini na serikali ya Saudi Arabia kuhusu harakati za kupata amani nchini humo.

Uamuzi wa kundi la STC unachochea mogogoro wa kivita kati ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ukiisaidia serikali inayotambuliwa kimataifa dhidi ya waasi wa Houthi ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Kaskazini.

Kundi la STC linalodai uhuru wa Kusini mwa Yemen kutoka kwa Kaskazini limeituhumu serikali kwa ufisadi na kuchelewesha kwa makusudi utekelezaji wa makubaliano ya kugawana madaraka yaliyosimamiwa na Saudi Arabia na kusainiwa Novemba mwaka jana katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen ,Mohamed al-Hadhrami, amekana madai hayo ya STC.

Wakati huo huo Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia imeonya kuhusu matokeo mabaya kabisa dhidi ya hatua ya kundi linalotaka kujitenga kusini mwa nchi hiyo lililotangaza kuanzisha utawala binafsi katika maeneo yaliyoko chini ya udhibiti wake nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.