Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-SYRIA-USALAMA

Baraza la Wawakilishi latambua mauaji ya kimbari ya raia kutoka Armenia

Wiki tatu baada ya Uturuki kuzindua operesheni ya kijeshi dhidi ya vikosi vya Kikurdi nchini Syria, Baraza la Wawakilishi nchini Marekani Jumanne (Oktoba 29) limetambua mauaji ya kimbari ya raia kutoka Armenia katika kura ya kipekee.

Wanawake wakikusanyika kwenye Ukumbusho wa mauaji ya Kimbari ya raia wa Armenia Yerevan Aprili 21, 2015.
Wanawake wakikusanyika kwenye Ukumbusho wa mauaji ya Kimbari ya raia wa Armenia Yerevan Aprili 21, 2015. REUTERS/David Mdzinarishvili
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Uturuki imesema kuwa imeghadhabishwa na msimamo huo wa Baraza la Wawakilishi la Marekani.

Matokeo ya kura yalipokelewa kwa shangwe na vigelegele. Azimio la kutambua mauaji ya kimbari ya raia kutoka Armenia yalipitishwa na idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha Democratic na wale kutoka chama cha Republican katika Baraza la Wawakilishi.

Kura ambayo inapigwa wiki chache baada ya vikosi vya Marekani kujiondoa na Uturuki kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi Kaskazini mwa Syria. Hali ambayo imesababisha ukosoaji mkubwa hata katika kambi ya washirika wa karibu wa wa Donald Trump.

Kwa upande wa mbunge kutoka chama cha Democratic Adam Schiff ambaye alitetea nakala hiyo ya kutambuliwa mauaji ya kimbari ya raia kutoka Armenia na Dola la Ottoman, amesema ilikuwa muhimu kutuma ujumbe mkali katika muktadha wa sasa kwa serikali ya Ankara. "Tunapoona picha za familia ilizokandamizwa Kaskazini mwa Syria, hatuwezi kusema kwamba uhalifu wa karne iliyopita ni jambo la zamani. Hatutasahau, na hatutakaa kimya, " amesema Adam Schiff.

Wabunge pia wamepitishwa kwa idadi kubwa vikwazo dhidi ya maafisa wengine wa Uturuki kuhusiana na mashambulizi nchini Syria.

Azimio hilo halikuifurahisha Uturuki. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imelaani vikali kile ilichokiita "kitendo cha kisiasa kisicho na maana" na kutaka tu"kuiridhisha Armenia na makundi yanayopambana dhidi ya Uturuki". Ankara inakataa kutumia neno la mauaji ya kimbari na inaendelea kusem akuwa yalikuwa mauaji kama mauaji mengine yaliyotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na pande zote zilipoteza wakati huo wa vita.

Mauaji ya kimbari ya raia wa Armenia yanatambuliwa na nchi thelathini na jamii ya wanahistoria. Kulingana na makadirio, kati ya Waarmenia milioni 1.2 na milioni 1.5 waliuawa wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia na askari wa Dola ya Ottoman, wakati huo ilikuwa msirika wa Ujerumani na Austria na Hungary. Hata hivyo Rais Trump, yeye mwenyewe hajawahi kutumia neno la mauaji ya kimbari.

Dola ya Ottoman ilikuwa mojawapo ya Ufalme mkubwa zaidi wa Dunia

Milki ya Osmani (pia: Ottomani) ilikuwa dola kubwa lililotawala upande wa mashariki wa Mediteranea pamoja na nchi nyingi za Mashariki ya Kati kati ya karne ya 14 na mwaka 1922.

Milki ilianzishwa na Waturuki Waosmani ikachukua nafasi ya ukhalifa wa Waabbasi na Milki ya Bizanti.

Mji wake mkuu ulikuwa Konstantinopoli (leo: Istanbul) na mtawala wake mkuu alikuwa Sultani wa Waosmani. Imani rasmi ya milki ilikuwa Uislamu hata kama katika maeneo mengi idadi kubwa ya wakazi walikuwa Wakristo.

Tabaka la viongozi wa kisiasa na wa kijeshi walikuwa Waosmani waliokuwa Waturuki pamoja na mchanganyiko wa Waislamu kutoka sehemu zote za milki yao, hasa Balkani

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.