Pata taarifa kuu
SYRIA-MAREKANI-UTURUKI-USALAMA

Syria: Putin akutana na Erdogan ambaye anatishia kuanzisha tena mashambulizi

Rais wa Urusi Jumanne wiki hii amempokea mwenzake wa Uturuki na wamejadili kuhusu mazungumzo yanayohusu mapigano kaskazini mashariki mwa Syria.

Rais wa Uturuki Erdogan na Rais wa Urusi Putin wamekutana  Sochi Jumanne, Oktoba 22 kabla tu ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano katika mashambulizi ya Uturuki nchini Syria.
Rais wa Uturuki Erdogan na Rais wa Urusi Putin wamekutana Sochi Jumanne, Oktoba 22 kabla tu ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano katika mashambulizi ya Uturuki nchini Syria. Reuters/Mustafa Kamaci/Turkish Presidential Press Office/
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo serikali ya Ankara imetishia kuanza tena mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi kabla tu ya kumalizika kwa muda wa kusitisha mapigano.

"Hali katika kanda hii ni mbaya sana," Vladimir Putin amesema mwanzoni mwa mkutano wake na Recep Tayyip Erdogan, akimtaka "kupata suluhisho hata kwa maswala magumu zaidi".

Alipowasili Sochi, Erdogan amesema ana matumaini kuwa mazungumzo hayo yatakuwa na "nafasi thabiti kwa kudumisha amani" kwani Ankara inataka wapiganaji wa Kikurdi kuondoka kaskazini mashariki mwa Syria, pamoja na katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali ya Syria inayoungwa mkono na Moscow.

Hivi karibuni, Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu, alifahamisha kwamba sio kusitisha mapigano bali ni “kuwapa muda wapiganaji wa PYD tawi la kundi la kigaidi la PKK kuondoka katika mipaka ya Uturuki na Irak na Syria.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki alisema kuwa makubaliano na tume hiyo kutoka Marekani kuhusu PYD ni kuwapokonya silaha nzito na kuondoa kambi zao wanazotumia kushambulia Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.