Pata taarifa kuu
ISRAELI-UCHAGUZI-SIASA

Waisraeli wanapiga kura kuamua hatma ya Netanyahu

Wananchi wa Israeli wanapiga kura leo Jumanne katika uchaguzi wa wabunge unaowapambanisha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, madarakani kwa muongo mmoja, na mkuu wa zamani wa jeshi Benny Gantz, miezi mitano baada ya duru ya kwanza bila kupatikana mshindi yeyote.

Uchaguzi wa bunge nchini Israeli Jumanne hii Septemba 17 unawakutanisha Benyamin Netanyahu na Benny Gantz.
Uchaguzi wa bunge nchini Israeli Jumanne hii Septemba 17 unawakutanisha Benyamin Netanyahu na Benny Gantz. RONEN ZVULUN, Jack GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vituo vua kupigia vimefunguliwa saa 07:00 saa za Israeli (sawa na saa 04:00 saa za kimataifa) na vitafungwa saa nne kamili usiku saa za Israeli (sawa na saa moja kamili Usiku saa za kimataifa) kwa kinyang'anyiro hiki cha duru ya pili.

Wapiga kura milioni 6.4 wanapiga kura katika vituo vya kupigia kura 10,700. Mapema leo Jumanne asubuhi katika moja ya vituo vya kupigia kura katika mji wa Jerusalem, hali ilikuwa shwari, na watu wachache tu ndi walionekana wakija kupiga kura, mwandishi wa habari wa shirika la Habari la AFP amesema.

Mnamo mwezi Aprili, chama cha Likud (cha mrengo wa kulia) cha Bw Netanyahu na chama cha mrengo wa kati, Kahol Lavan, cha Bw. Gantz vilipata kila upande viti 35 kwa jumla ya viti 120 katika Bungela Knesset.

Baada ya uchaguzi huo Rais wa Israeli Reuven Rivlin alimwagiza Benjamin Netanyahu kuunda serikali ya muungano. Jambo ambalo, Bwana Netanyahu alishindwa na kuamua kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anakabiliwa na kibarua kigumu katika Uchaguzi huu ambao iwapo chama chake kitashinda, ataendelea kuwa Waziri Mkuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi katika historia ya nchi hiyo licha ya shutuma za ufisadi zinazomkabili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.