Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN-USALAMA

Mgombea katika uchaguzi wa wabunge auawa Afghanistan

Mgombea katika uchaguzi wa wabunge nchini Afghanistan ameuawa leo Jumatano katika mlipuko wa bomu lililotegwa chini ya kiti katika ofisi yake katika jimbo la Helmand kusini mwa nchi hiyo.

Mashambulizi ya Taliban yameua watu wengi nchini Afghanistan.
Mashambulizi ya Taliban yameua watu wengi nchini Afghanistan. AZEEM ZMARIAL/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Abdul Jabar Qahraman, ambaye alikuwa anawania katika uchaguzi a wabunge uliopangwa kufanyika siku ya Jumamosi, ameuawa na wengine saba wamejeruhiwa, msemaji wa serikali ya mkoa amesema.

Kundi la Taliban, ambalo hivi karibuni lilitoa wito wa kususia uchaguzi huo, limedai kuhusika na shambulio hilo.

"Bomu liliwekwa chini ya kiti cha Qahraman katika ofisi yake ya kampeni, Tunachunguza tukio hilo," msemaji huyo wa serikali ay mkoa ameongeza.

Qahraman ni mgombea wa kumi katika uchaguzi wa wabunge anauawa ndani ya miezi miwili. Wengine wawili walitekwa nyara na wanne walijeruhiwa na wanamgambo wa Kiislamu.

Wiki iliyopita, watu 22 waliuawa katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi katika Jimbo la Takhar kaskazini mashariki mwa Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.