Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Mapigano yaendelea kurindima Ghouta Mashariki, Syria

Muda wa saa tano wa usitishwaji mapigano uliotolewa na rais wa Urusi Vladimir Putin haukuheshimishwa leo Jumanne asubuhi katika eneo la Ghouta mashariki, linaloshikiliwa na waasi, mashariki mwa Damascus.

Ghouta mashariki yaendelea kukumbwa na mashambulizi.
Ghouta mashariki yaendelea kukumbwa na mashambulizi. Ammar SULEIMAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi mapigano makali yanayoendelea yamekwamisha operesheni ya kuondoa raia wa kawaida katika eneo hulo na kusafirisha msaada wa kibinadamu kwa walengwa.

"Ni jambo la kufa au kupona, tunahitaji usitishwaji wa mapigano kwa muda wa siku thelathini nchini Syria, kama ilivyodaiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa," amesema Jens Laerke, msemaji wa Tume ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wanachama kumi na tano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walipitishwa siku ya Jumamosi bila kupingwa azimio linalotoa wito "bila kuchelewa" wa usitishwa mapigano wa siku thelathini kwa minajili ya kutoa huduma kwa raia waliokwama katika eneo la Ghouta mashariki.

Katika ziara yake nchini Urusi siku ya Jumanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, alisisitiza kuwa Urusi ni "mmoja wa wachangiaji wa kimataifa ambao inaweza kusikikakuhusu kutekelezwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa". .

Katika mkutano na waandishi wa habari na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, Jean-Yves Le Drian alisema makundi matatu ya waasi nchini Ghouta mashariki yalithibitisha nia yao ya kuheshimu muda huo uliotolewa wa kusitisha mapigano.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov, ameshtumu waasi wa Syria kuwashikilia raia mateka na kuzuia kuundwa kwa "Njia ya Kihisani" kwa kuwahamisha raia waliokwamama katika eneo la Ghouta mashariki.

Kwa mujibu wa serikali ya Damascus na jeshi la Urusi, waasi waliendesha mashambulizi kwenye barabara ambayo ingelitumiwa na raia kwa kuondoka eneo hilo la mapigano.

Mamia ya watu wamepoteza maisha baada ya kuanza kushambulia eneo la Ghouta mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.